Boti iliyobeba Timu na Mashabiki yazama Uganda Baadhi ya wasiojua kuogelea wafa maji Ziwa Albert

screen-shot-2016-12-27-at-10-43-33-am

Taarifa za kipolisi kutoka nchini Uganda zimeeleza kuwa boti lililokuwa limebeba timu ya mpira wa miguu pamoja mashabiki wake lilipinduka na kuzama katika Ziwa Albert.

Zaidi ya watu 30 ambao ni miongoni mwa 45 waliokuwamo katika chombo hicho walizama, huku wengine 15 wakielezwa kujiokoa kwa kuogelea kutoka katika tukio hilo lililotokea umbali wa mita 100 hadi eneo la pwani ya karibu.

Jitihada za wavuvi wanaoendesha shughuli zao katika ziwa hilo zilikuwa msaada mkubwa kwa jeshi la uokoaji ili kunusuru baadhi ya waliozama.

Kuhusu sababu za kuzama kwa boti hilo, jeshi la polisi limezitaja kuwa ni pamoja na kubeba abiria kupita kiasi hali iliyopelekea kuzidiwa uwezo hatimaye kuzama.

Timu ya kijiji cha Kaweibanda kutoka wilaya ya Buliisa ilikuwa ikisafiri na mashabiki wake kwenda ng’ambo ya ziwa Albert katika wilaya Hoima kwa ajili ya mechi ya kirafiki ikiwa ni desturi yao kila ifikapo msimu wa sikukuu za Krismas.

Mkuu wa jeshi la Polisi wa Wilaya ya Buliisa John Rutagira amesema miongoni mwa miili ya watu 9 waliopoteza maisha alikuwemo pia shabiki mwanamke mwenye miaka 18 aitwaye Consolate Akutu ambaye anadaiwa kuwa na mtoto mwenye miezi 5 ambapo alimwacha nyumbani kwa wazazi wake.

Facebook Comments