Manispaa ya Ilala yatiliana saini na mkandarasi, Ujenzi wa Barabara za Michepuko na Mifereji

screen-shot-2016-12-31-at-7-28-18-pm

Manispaa ya Ilala jijini dar es salaam jana imetiliana saini na kampuni ya Railway 7th Group kutoka china mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara 5 za michepuko na mifereji chini ya ufadhili wa benki ya dunia lengo likiwa kusaidia kukabiliana na changamoto za miundombinu katika jiji hilo lenye takriban wakazi milioni tano .

Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiwaji saini wa mkataba huo utakaogharimu shilingi bilioni 11.1 mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa hivyo amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo kwa umakini kulingana na thamani ya fedha lakini pia imalizike kwa wakati.

Awali mratibu wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya jiji la dar es salaam DMDP upande wa manispaa ya Ilala Celestina Magesa amezungumzia maeneo ambayo mradi huo umelenga kutekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara na mitaro, kuboresha maeneo yasiyofikika ili yaweze kupata huduma, kuzijengea uwezo taasisi pamoja na usimamizi wa miradi na tathmini.

Facebook Comments