Tanzania na Ethiopia zasaini mikataba 15

Waziri Mkuu wa Ethiopia HAILEMARIAMU DESALEGN amewasili leo nchini na kupokelewa na mwenyeji wake rais John Pombe Magufuli, wakiwa Ikulu jijini dar es salaam pamoja na mazungumzo ya faragha, pia wamesaini mikataba 15 ambayo inalenga kukuza uchumi wa nchi hizo mbili. Miongoni mwa mikataba iliyosainiwa na Waziri Mkuu huyo wa Ethiopia ni pamoja na ule[…]

Kesi ya Ufisadi Korea Kusini, Aliyekuwa Rais wa nchi hiyo akamatwa

Aliyekuwa rais wa Korea Kusini Park Geun-hye amekamatwa kuhusiana na madai ya rushwa ambayo yalisababisha kuondolewa kwake madarakani. Waendesha mashtaka wanaweza kumuweka mahabusu kwa muda wa hadi siku 20 kabla ya kumfungulia mashtaka rasmi. Rais huyo wa zamani wa Korea Kusini anakabiliwa na madai ya kushirikiana na rafiki yake aliyewalazimisha wafanya biashara wakubwa kutoa fedha[…]

Hali ya Kisiasa nchini Congo,Upinzani kuitisha maandamano makubwa

Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeitisha maandamano kote nchini humo siku ya Jumatatu wiki ijayo, lakini pia inawataka watu kutokwenda kazini ili kumshinikiza rais Joseph Kabila kutekeleza mkataba wa kisiasa uliotiwa saini mwishoni mwa mwaka 2016. Muungano huo wa Rassemblement umesema kuwa utahakikisha kuwa shughuli za kila siku katika miji yote nchini humo[…]

Mgogoro wa Kisiasa Afrika Kusini, Rais Jacob Zuma awafuta kazi baadhi ya mawaziri wake

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewafukuza kazi mawaziri wake kadhaa akiwemo Waziri wa fedha Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio waliokua sababu kuu ya kuwepo mabadiliko haya. Taarifa kutoka ikulu ya Afrika Kusini zinasema Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Pravin Gordhan. Takriban[…]