Watu wanaojihusisha na uvuvi haramu kuchukuliwa hatua kali za kisheria Ukerewe Mwanza

Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, imeonya kuwachukulia hatua kali za kisheria, watu wanaojihusisha na upunguzaji wa vipimo vya nyavu za kuvulia Samaki vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria, ili kuhalalisha uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria. Ni wingu zito la moshi mweusi likiashiria kuteketezwa kwa shehena ya Nyavu za uvuvi haramu, zilizokuwa zikitumika katika[…]

ATCL imefufua safari zake za ndege kutoka Mtwara – Dar kwa kutumia ndege mpya aina ya Bombardier

Shirika la ndege ATCL limefufua safari zake za ndege kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa kutumia ndege mpya aina ya bombardier zilizonunuliwa na serikali kwa lengo la kulifufua shirika hilo. Ni ndege mpya aina ya bombardier ikiwasili mkoani Mtwara ni mda mrefu ndege za serikali za ATCL hazijatua katika uwanja huu. Kuanza kwa safari[…]

Kwa muda mrefu wakazi wa Kata ya Mahango Bariadi wamekuwa wakitumia usafiri wa mikokoteni kuwapeleka wagonjwa hospitalini

Zaidi ya Wakazi Elfu 53 wa Kata ya Mahango katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu wameondokana na adha ya muda mrefu ya kutumia usafiri wa mikokoteni inayokokotwa na ng’ombe pamoja na baiskeli kuwapeleka wagonjwa wao katika vituo vya afya vya karibu pamoja na Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, baada ya kupatiwa gari[…]

Mwendesha Boda Boda auwawa kwa kukatwa sehemu za siri, wauaji watoweka nazo Geita

WATU wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti ndani ya wiki moja wilayani Geita mkoani Geita akiwemo mwendesha bodaboda na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ndize Gabriel (40) mkazi wa Mtaa wa Katoma mjini Geita aliyekatwa sehemu mbalimbali za mwili wake zikiwemo sehemu za siri huku wauaji hao wakitoweka nazo. Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo kamanda[…]

Siku 100 za rais Trump, Ajivunia mafanikio aliyoyapata licha ya changamoto

Rais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku mia moja tangu aingie madarakani kwa kutoa hotuba ambayo hata hivyo imedaiwa kuwashambulia wanahabari na kutetea mafanikio yake. Bwana Trump amewaaambia wafuasi wake huko Pennsylvania kwamba ameridhika kuwa pamoja nao badala ya kuhudhuria dhifa ya chakula cha jioni na wanahabari hao iliyokuwa ikifanyika katika ikulu ya White House[…]