Ugonjwa wa mnyauko wa mikorosho waanza kuenea kwa kasi

Watafiti wa zao la korosho kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo naliendele mkoani Mtwara wamesema kasi ya kuenea kwa ugonjwa mpya wa mnyauko wa mikorosho imeongezeka ambapo wamewataka wakulima kufuata ushauri wa watalaam hao huku wakiendelea kusubiri dawa ya ugonjwa huo ambao kwa sasa haijapatikana. Daktari Fortunus Kapinga ni mtafiti kiongozi wa zao la korosho[…]

Mgodi wa dhahabu Magunga, Wachimbaji wadogo waomba kuchimba

Baadhi ya wachimbaji wadogo katika mgodi wa dhahabu uliopo Magunga wilayani Butiama mkoani Mara wameiomba serikali iwaruhusu kuendelea na shughuli za uchimbaji kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya kimaisha. Ombi la wachimbaji hao limekuja ikiwa ni miezi sita tangu serikali ilipoufunga mgondi huo kufuatia janga la watu sita kupoteza maisha baada ya kuangukiwa na[…]

Mzee wa miaka 85 afunga ndoa, jamii yaaswa

Imeelezwa kuwa ndoa nyingi zinasambaratika kutokana na wanandoa wengi kukosa maadili na mapokeo ya kiimani kwa wanandoa wengi kuiga tabia zilizoko katika mitandao ya kijamii na kuacha imani zao, maadili ya ndoa na maadili ya jamii. Hayo yemeelezwa katika sherehe ya ndoa ya mzee wa miaka 85 ambaye amefunga ndoa na Mjane wa miaka 34[…]

Miundombinu ya Gesi asilia Kujengwa Dodoma, Mwanza, Tanga, Mbeya na Arusha

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC linakusudia kuanza utafiti wa namna ya usambazaji wa miundombinu ya kusafirishia gesi asilia kwenye mikoa ya Dodoma, Mwanza, Tanga, Mbeya na Arusha. Hatua hiyo inakwenda sambamba na kuandaa mpango kabambe wa mtandao wa miundombinu ya Gesi asilia mkoani Pwani ili kuwezesha viwanda vitakavyojengwa mkoani humo viweze kutumia gesi[…]

Tanzania yatishia kufuta usajili kwa waendeshaji utalii wasio waaminifu

Serikali ya Tanzania imetishia kufuta usajili kwa kampuni za kusafirisha watalii zinaozokwenda kinyume na sheria na kanuni za sekta ya utalii za Tanzania. Onyo hilo limetolewa na waziri ya Maliasili na Utalii wa Tanzania Prof Jumanne Maghembe kwa watu wasiofuata maadili, na wanaowahadaa watalii wanaotaka kwenda kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania. Prof Maghembe amemuagiza[…]