Serikali kutumia Drones Kusambazia dawa kwenye maeneo magumu kufikika

Serikali inakusudia kutumia ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kusambaza dawa muhimu za binadamu kwenye vituo vya afya vya umma vilivyopo kwenye maeneo yenye changamoto ya kufikika kwa urahisi. Mpango huo utakaoanza mwakani, utaanzia kwenye zahanati na vituo vya afya vya serikali elfu moja vilivyopo mkoani Dodoma kabla ya kusambazwa kwenye mikoa kumi iliyopo[…]

Daladala yagonga treni Morogoro, Watu watatu wapoteza maisha na wengine 31 wajeruhiwa

Wanafunzi wawili wa shule ya sekondari wamethibikika kuwa miongoni mwa watu watatu waliopoteza maisha ambapo watu wengine 31 wamejeruhiwa baada ya basi aina ya coaster maarufu kama daladala lenye namba za usajili T 438 ABR kugonga treni ya abiria iliyokuwa inatoka Mwanza kwenda Dar es Salaam majira ya saa 1:30 asubuhi mjini Morogoro Majeruhi wamefikishwa[…]

Barcelona yapanga kumshtaki Neymar, yataka ilipwe Pauni milioni 7.8 Klabu ya Barcelona imepanga kumshitaki Neymar ikidai ilipwe pauni milioni 7.8

Klabu hiyo inaamini kuwa Neymar alikiuka makubaliano ya mkataba wakati akihamia PSG aliyojiunga nayo kwa kitita cha pauni milioni 198. Barcelona inataka ongezeko la asilimia 10 katika mauziano hayo ikisisitiza inatakwa ilipwe. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil alivunja rekodi ya uhamisho kwa kitita cha pauni milioni 200 kwa timu hiyo ya Ufaransa mnamo mwezi[…]

Kenya na Tanzania kufanya mazungumzo kuondoa vikwazo vya kibiashara (Picha Maktaba)

Kenya na Tanzania zinapanga kufanya mazungumzo mwezi ujao ili kuondoa vizuizi vya kibiashara. Katibu mkuu wa wizara ya viwanda, biashara na ushirikiano ya Kenya Bw Chris Kiptoo amesema mazungumzo hayo yatakayofanyika nchini Tanzania ni mchakato unaofuata mazungumzo yaliyofanyika awali, ya kutatua hali ya kukwamakwenye biashara ya ngano na gesi. Amesema nchi hizo mbili zina nia[…]