Mwaka mpya wa kiislamu, Wito watolewa kutenda mema

Katika hatua nyingine, Uongozi wa shule ya Shekhat Hissa Islamic Seminary kwa kushirikiana na walimu wa shule hiyo leo umeungana na waislamu wote duniani katika kusheherekea kuukaribisha mwaka mpya wa kiislamu ambao ni mwaka 1439 hijiria. Mbali na kufanya maandamano yaliyoshirikisha wanafunzi, pia ulitoa elimu elekezi kwa jamii ya watu wa kada mbalimbali juu ya[…]

Mkazo masomo ya sayansi shule za sekondari, Walimu Ubungo,Dsm,wabadilishana mbinu shirikishi za Ufundishaji

Walimu zaidi ya mia moja wa Masomo ya Sayansi kwa Shule za Sekondari za Serikali Wilaya ya Ubungo,Mkoani Dar Es Salaam,wamesema dhana kuwa masomo ya sayansi ni magumu,inatokana na masomo hayo kutokuwa katika mfumo shirikishi na kwamba umefika wakati sasa,masomo hayo kufundishwa katika mfumo huo. Baadhi ya walimu hao,wameimbia Channel Ten,katika mahojiano maalum,wakati wa mafunzo[…]

Sakata la mwekezaji stendi ya Makumbusho, Serikali yamuamuru kulipa deni la Milioni 79 ndani ya mwezi mmoja

Serikali wilaya ya Kinondoni,imetoa mwezi moja kwa mwekezaji wa stend ya makumbusho,Dar Es Salaam, pamoja na jengo la ghorofa lilopo katika stend hiyo, kulipa shilingi milioni 79 ambazo anadaiwa na manispaa ya kinondoni ama la akishindwa manispaa isitishe mkataba wake alioukiuka. Mkuu wa Wilaya hiyo, ALLY HAPI, akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wafanyabiashara[…]

Umoja wa Mataifa Kuwatuma wachunguzi Yemen

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limekubali kuwatuma wachunguzi wa uhalifu wa kivita nchini Yemen, na hivyo kushinda pingamizi kutoka kwa Saudi Arabia lililopinga kuruhusu uchunguzi huru wa kimataifa. Katika makubaliano hayo yaliyoafikiwa kwa pamoja, baraza hilo limemtaka mkuu wa haki za kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein kutuma[…]

Cameroon yapiga marufuku Mikutano maeneo yanayozungumza Kiingereza

Maafisa nchini Cameroon hapo wamepiga marufuku kwa siku tatu mfululizo, mikutano yoyote ya kuanzia watu wanne na zaidi, katika mkoa wake unaozungumza lugha ya Kiingereza. Aidha wameamuru kufungwa kwa vituo vya mabasi, migahawa na maduka na kupiga marufuku mizunguko ya watu katika maeneo ya mkoa huo. Hatua hiyo inalenga kuzuia maandamano ambayo yamepangwa na Wacameroon[…]

Watoto Milioni tatu Nigeria Wakosa masomo sababu ya Boko Haram

Machafuko yanayoendelezwa na wanamgambo wa Boko Haram Kaskazini mwa Nigeria yamelazimisha asilimia 57 za shule katika jimbo la Borno kufungwa, hali ambayo imewaacha wanafunzi milioni tatu bila masomo wakati ambapo shule zinafunguliwa. Hayo yameelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF. Baada ya kumaliza ziara ya siku tatu katika eneo la Maidiguri ambalo[…]