Hukumu ya Manji Oktoba 06, 2017, Ushahidi wa kutumia dawa za kulevya wafungwa

Mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu Dar Es Salaam, leo imefunga kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi iliyokuwa inamkabili mfanyabiashra Yusuph Manji ya kutumia dawa za kulevya, na kutarajiwa kutoa hukumu ya shauri hilo Oktoba sita mwaka huu. Mahakama hiyo awali imekataa kupokea kielelezo cha cheti cha Daktari kutoka nchini Marekani,kuhusiana na dawa[…]

Uchunguzi wa Shambulio la Lissu, Serikali yasisitiza watanzania kuviamini vyambo vya dola

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesema msimamo wa serikali kuhusiana na tukio la kupigwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu halitachunguzwa na vyombo vya uchunguzi vya nje, na kwamba vyombo vya dola vya ndani ndivyo vinavyohusika na uchunguzi huo. Amesema tukio hilo na matukio mengine yaliyojitokeza hayana sababu ya[…]

Baada ya uchaguzi nchini Ujerumani, Kansela Merkel kuzungumza na chama za SPD

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema anakusudia kuwa na mazungumzo na chama cha Social Democrats (SPD) kuhusiana na uwezekano wa vyama hivyo kuunda serikali ya pamoja ingawa tayari kiongozi wa chama hicho Martin Schulz amesema chama cha SPD hakiko tayari kuwemo katika serikali ya pamoja bali kitakuwa chama cha upinzani. Kansela Merkel amesema atafanya mazungumzo[…]

Vita ya maneno kati ya Marekani na North Kores, Korea kaskazini yasema ujumbe wa Trump unaashiria tangazo la Vita

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini amesema kuwa ujumbe wa Rais Donald Trump wa mwishoni mwa wiki katika ukurusa wa twitter ulikuwa unaashiria “tangazo la vita.”. Mwanadiplomasia huyo amesema licha ya ujumbe huo, Trump pia alidai kuwa uongozi wa Korea Kaskazini hautasalia madarakani kwa muda mrefu na mwishoe akatoa kauli kama hiyo ya[…]

Uteuzi wa Rais mpya wa Angola, Joao Lourenco aapishwa kushika madaraka

Rais mpya wa Angola ameapishwa leo ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika mabadiliko katika uongozi wa taifa hilo katika kipindi cha miongo karibu minne. Jo„o LourenÁo, (TAMKA JOE RAURANSO) aliyekuwa waziri wa ulinzi anachukuwa nafasi ya Jose Eduardo Dos Santos rais anayeondoka ambaye aliamua kuachia madaraka baada ya kuongoza miaka thalathini na nane. Bwana LourenÁo[…]

Ligi kuu Uingereza (EPL): Chelsea, Man U, Man City na Tottenham zafanya vyema.

Kwa mara ya kwanza katika msimu huu Alvaro Morata anapiga Hat-Trick na kuisaidia Chelsea kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Stoke City. Katika mechi ya Tottenham na West Ham hadi mchezo unamalizika, Tottenham waliibuka na ushindi wa goli 3-2. Nayo Manchester United imeifunga Southamton goli 1-0. Huku Manchester City wakiibamiza bila huruma Cystal[…]