Mradi wa Bwawa (W) Kisarawe, Jumla ya shs bil. 1.5 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI Seleman Jaffo amesema jumla ya shilingi bilioni moja na nusu zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa bwawa la maji wilayani Kisarawe unaotarajiwa kukamilika desemba mwaka huu. JAFFO amebainisha hayo wilayani kisarawe mkoani Pwani akiwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kukagua[…]

Wabunge wa Chadema Godbless Lema na Joshua Nassari wafika ofisi za TAKUKURU kukabidhi ushahidi wa Video

Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Godbless Lema, wa Arusha Mjini pamoja na Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki leo wamefika katika Ofisi za Kuzuia na kupambana na rushwa PCCB jijini Dar es Salaam kuwasilisha kinachodaiwa kuwa ushahidi wa picha za video unaoonyesha jinsi baadhi ya Madiwani wa Chama hicho mkoani Arusha walivyoshawishiwa kukihama[…]

Kura ya maoni uhuru wa Catalonia, Kiongozi wa eneo hilo atangaza ushindi

Kiongozi wa neo la Catalonia Carles Puigdemont anasema kuwa eneo la Uhispania limepata haki ya kuwa huru kufuatia kura ya maoni yenye utata ambayo imekubwa na ghasia ambapo kiongozi huyo amesema sasa mlango umefunguliwa kwa eneo hilo kutangazwa kuwa huru. Maafisa wa Catalonia baadaye walisema kuwa asilimia 90 ya wale walioapiga kura waliunga mkono uhuru[…]

Shambulizi mjini Las Vegas Marekani, Watu ishirini wameuawa na wengine mia moja kujeruhiwa

Watu ishirini wameuawa na huku wengine zaidi ya mia moja wakiripotiwa kujeruhiwa baada ya mtu asiyefahamika kufyatua wa risasi wakati wa tamasha moja huko Las Vegas Marekani. Mtu huyo mwenye silaha alifyatua risasi katika tamasha la muziki kwenye hoteli ya Mandalay Bay mjini humo. Mamia ya watu walikuwa wakikimbia ovyo kwenye eeo hilo baada ya[…]

Waasi watano wauawa kaskazini mwa Algeria

Taarifa iliyotolewa na wizara ya ulinzi wa Algeria imesema vikosi vya kupambana na ugaidi vya Algeria vimewaua waasi watano kwenye eneo la El Kseur mkoani Bejaia. Habari zimesema bunduki tano aina ya Kalashnikov pamoja na magazini tatu zilikamatwa katika opresheni hiyo. Mbali na hayo, Alhamisi ya wiki iliyopita vikosi vya jeshi vilianza opresheni kubwa katika[…]