Kukamilika Chaguzi za Ndani CCM Mbarali, Viongozi waliochaguliwa kujengewa uwezo kwa mafunzo

CHAMA cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kimejipanga kutoa mafunzo ya uongozi kwa viongozi wote waliochaguliwa baada ya chaguzi za ndani ya chama hicho kumalizika, lengo likiwa kuwajengea uwezo wa kiutendaji kwenye nafasi zao. Katibu wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali Abdalah Mpokwa anatoa kauli hii wakati wa chaguzi za Jumuiya ya Wazazi,[…]

Mgogoro wa Ardhi Kigamboni, Mwekezaji atakiwa kurudisha kwa wananchi sehemu ya ardhi

Mkuu wa Willaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa amemtaka mwekezaji wa mradi wa Nyumba wa AVIC TOWN Kigamboni jijini Dar es Salaam kurudisha kwa wananchi eneo la ardhi analodaiwa kulitwaa kutoka kwa wananachi hao wa Somangila kufuatia malalamiko waliyomfikishia kuhusu mgogoro huo. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mipaka ya ardhi katika eneo la mradi wa nyumba[…]

Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, Chajipanga kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko

Serikali imepongeza uzalishaji wa sukari katika kiwanda cha sukari Mtibwa Mkoani Morogoro ambao umetia hamasa na imani ya kukabiliana na changamoto ya upungufu wa sukari uliokuwa ukiongelewa mara kwa mara hususan kutokana na kiwanda hicho kujipanga kuzalisha sukari kwa kiwango cha juu kufuatia uwepo wa soko la uhakika hapa nchini. Akiongea na uongozi wa kiwanda[…]

Rais Dkt John Pombe Magufuli amezitaka Halmashauri nchini kuendelea kudhibiti mianya ya Upotevu wa mapato

Rais Dkt John Pombe Magufuli amezitaka Halmashauri nchini kuendelea kudhibiti mianya ya Upotevu wa mapato na Ubadhirifu, watumishi wa sio waadilifu katika halmashauri zao huku akizipa changamoto ya kubuni mbinu za kuongeza mapato ili kuwaletea maendeleo wananchi. Akifungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania -ALAT Rais Magufuli amesema serikali ya[…]

Kujitenga kwa jimbo la Catalonia, Mgomo mkubwa waitishwa na vyama vya wafanyakazi

Shughuli nyingi zinatazamiwa kukwama katika eneo la Catalonia kufuatia mgomo mkubwa ulioitishwa na vyama vya wafanyakazi kulalamikia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ulioshuhudiwa siku ya Jumapili wakati wa kura ya maoni ya kujitawala. Wafanyakazi wameapa kutoripoti leo kazini na baadhi ya maduka na sehrmu mbalimbali za starehe kufungwa. Wakati wa zoezi hilo siku ya[…]

Polisi nchii Marekani wanaendelea kufanya uchunguzi kina kujua sababu ya ufyatuaji mkubwa wa risasi

Polisi nchii Marekani wanaendelea kufanya uchunguzi kina kujua sababu ya ufyatuaji mkubwa wa risasi uliosababisha vifo vya watu 59 na kuwajehi wengine 527 kwenye tamasha moja huko Las Vegas nchni Marekani. Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64, alimimina risasi kutoka ghorofa ya 32 ya hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwenye umati wa watu waliokuwa[…]

Machafuko Cameroon, Shirika la Amnesty international lataka kufanyika uchunguzi

Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limerudia mwito wake wa kutaka uchunguzi ufanywe kuhusu vifo vya waandamanaji wanaounga mkono kujitenga kwa eneo linalozungumza Kiingereza nchini Cameroon. Habari zinasema kwamba watu wasiopungua 17 walipoteza maisha katika makabiliano baina ya polisi na waandamanaji hao. Ghasia zilitokea Jumapili katika maeneo mengi ya sehemu ya Kusini Magharibi[…]

Baada ya matokeo ya Urais kufutwa Kenya, Wagombea wote wa urais wakutana na tume ya uchaguzi

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amefika kwenye mkutano ulioitishwa na tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC katika ukumbi wa Bomas of Kenya mjini Nairobi. Rais Uhuru Kenyatta ambaye naye alialikwa kwenye mkutano huo na IEBC alitarajiwa kufika katika mkutano huo ambao tume ilitisha mkutano na wagombea hao wakuu wa urais kabla[…]