Ujenzi Hospitali ya Temeke DSM, Asilimia 80 ya jengo la kitengo dharura na upasuaji yakamilika

Ujenzi wa jengo la kitengo cha huduma za dharura na Upasuaji katika hospital ya Temeke jijini dsm unaofadhiliwa na Ubalozi wa Japan kwa gharama ya shilingi millioni 323 umekamilika kwa asilimia 80 huku changamoto ikiwa ni ya vifaa vya kisasa kwa ajili ya Utoaji huduma za Dharura na Upasuaji. Akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa[…]

Miili inayoopolewa Baharini, Jeshi la Polisi launda timu ya wataalam kuchunguza

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa Jeshi la polisi nchini limeunda timu ya wataalamu kupeleleza na kuchunguza miili ya watu inayoopolewa baharini siku za hivi karibuni ambayo imezua gumzo miongoni mwa wananchi. Jeshi hilo pia limewataka watu waliopotelewa na ndugu zao watoe taarifa polisi kitengo cha upelelezi ili wafanye uchunguzi[…]

VETA na fedha za Masurufu,Serikali yaitaka kurejesha takriban shilingi milioni 600

Serikali imeiagiza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kurejesha fedha za masurufu takriban shilingi milioni 600, na wafanyakazi watakaoshindwa kurejesha fedha hizo, wakatwe kwenye mishahara yao. Agizo hilo limetolewa mjini Dodoma, na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, wakati alipokutana na Menejimenti ya (VETA), ambapo amesisitiza wale wote waliotumia[…]

Kuwakamata na kuwaweka ndani watumishi, Waziri Mkuu Majaliwa apiga marufuku, ataka taratibu zifuatwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku tabia ya baadhi ya viongozi katika maeneo mbalimbali nchini kuwakamata na kuwaweka ndani watumishi wakiwemo wauguzi bila ya kufuata taratibu. Aidha amewataka wauguzi nchini kufanya kazi kwa weledi, uaminifu pamoja na kufuata maadili ya taaluma yao kwa kuwa maisha ya wagonjwa yako chini yao. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo[…]

Mahusiano ya kidiplomasia, Marekani yaitaka Cuba kuondoa baadhi ya wafanyakazi wake nchini humo

Marekani imeitaka Cuba kuondoa wafanyakazi 15 wa ubalozi wake mjini Washington kwa muda usiozidi siku saba, kufuatia madai kuwa Cuba imekuwa ikifanya mfululizo wa mashambulizi ambayo yaliathiri afya za wanadiplomasia 22 wa Marekani nchini Cuba mnamo miezi ya hivi karibuni. Hata hivyo hakukutolewa maelezo zaidi kueleza mashambulizi hayo yalikuwa ya aina gani. Waziri wa Mambo[…]

Kujitenga kwa Catalonia Kiongozi wa jimbo hilo asema atatangaza ushindi

Kiongozi wa jimbo la Catalonia linalotaka kujitenga na Uhispania Carles Puigdemont ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC kwamba haitachukua muda mrefu kabla ya jimbo hilo kujitangazia uhuru wake, baada ya asilimia 90 ya watu milioni mbili waliopiga kura ya maoni yenye utata, kuunga mkono kujitenga. Kauli yake hiyo ilitolewa baada ya maelfu ya watu[…]

Taasisi ya elimu pamoja na Bodi ya Mikopo, Waziri Ndalichako azitaka kushughulikia taarifa za uchunguzi

Baraza la taasisi ya elimu Tanzania TET limetakiwa kuhakikisha linawachukulia hatua wahusika wote wa sakata la uandishi mbovu wa vitabu, na watumishi ambao hawana sifa kuwemo katika taasisi hiyo pamoja na kuhakikisha vitabu vilivyokuwa na makosa vinarekebishwa ili viweze kutoka. Agizo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa[…]

Uzinduzi wa Makumbusho ya Olduvai George Kuvutia watalii wengi na wanasayansi wa mambo ya kale

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi makumbusho ya Olduvai Gorge katika hifadhi ya Ngorongoro eneo pekee duniani ambapo inapatikana historia ya muda mrefu ya chimbuko la binadamu na hivyo kuwa moja ya kivutio kikubwa cha watalii nchini. Akizungumza katika uzinduzi huo, ulieonda sambamba na onyesho la kudumu la hatua za mabadiliko ya[…]