Operesheni ya kusaka Mifugo, Waziri aendesha operesheni kali Mwanga

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameendesha operesheni kubwa ya kusaka mifugo iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria katika Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro na kuonya kuwa kazi hiyo inayoendelea isihusishwe na ushirikiano mwema uliopo baina ya Tanzania na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Amesema watu watakaokamatwa katika operesheni hiyo watashughughulikiwa kwa mujibu[…]

Hali ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antipas Lissu imeendelea kuimarika tofauti na ilivyiokuwa awali

Hali ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antipas Lissu imeendelea kuimarika tofauti na ilivyiokuwa awali huku akiendelea na matibabu huko nchini Kenya. Akitoa taarifa kuhusu hali ya afya ya mbunge huyo,Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe amesema Lissu anaendelea vizuri na kwa sasa ameanza mazoezi baada ya kufanyiwa upasuaji mara 17.[…]

Shambulizi la bomu la kutegwa Somalia, Mamlaka za Usalama zaendelea kutafuta miili ya waliofunikwa na vifusi

Mamlaka za usalama nchini Somalia zimesema kwamba idadi ya watu waliouawa baada ya bomu kulipuka kwenye lori katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu mwishoni mwa wiki huenda ikawa zaidi ya tatu Shambulizi hilo linaelezewa kuwa baya zaidi kuwahi kutokea kwenye eneo lote la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo Takribani watu 400 walijeruhiwa[…]

Mchakato wa kuelekea uchaguzi wa marudio Kenya, Muungano wa NASA wasitisha maandaano kwa siku ya leo

Muungano wa Upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) umesitisha maandamano ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika nchini humo leo kushinikiza mabadiliko katika tume ya uchaguzi licha ya kwamba jana yalifanyika katika miji kadhaa ikiwemo Mombasa. Katika taarifa yake, muungano huo unaoongozwa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga umesema umechukua hatua hiyo kupata fursa ya kuomboleza[…]

Libya yarejesha wakimbizi haramu zaidi ya elfu 7

Ofisi ya kupambana na uhamiaji haramu ya mji wa Sabratha ulioko magharibi mwa Libya imesema, hivi karibuni serikali ya mji huo imewarejesha wakimbizi haramu 7,000 hivi. Ofisi hiyo imetoa taarifa ikisema, imeshirikiana na kikosi cha usalama cha mji wa Sabratha kukagua vituo vya kuwapokea wakimbizi haramu. Taarifa hiyo imefafanua kuwa, wakimbizi haramu 7,428 waliorejeshwa ni[…]

Ligi kuu Uingereza: Arsenal, Chelsea zachezea kichapo, Man City yafanya mauaji, Man U yaambulia sare.

Ligi kuu ya Uingereza (EPL) imeendelea wikiendi iliyomalizika huku Manchester City wakifanya mauaji kwa kuichapa Stoke City magoli 7-2. Crystal Palace imeilaza Chelsea kwa goli 2-1, huku Arsenal ikibomolewa na Watford kwa jumla ya magoli 2-1. Nayo Manchester United imeambulia sare ya 0-0 dhidi ya Liverpool. Share on: WhatsApp

Michuano ya Volleyball ya wanawake: Kenya, Cameroon zafuzu kushiriki kombe la dunia

Timu ya taifa za volleyball za wanawake za Kenya na Cameroon zimefuzu kushiriki fainali za kombe la dunia (FIVB) katika mashindano ya volleyball ya wanawake zitakazoandaliwa nchini Japan 2018. Malkia Strikers ya Kenya imejizolea tiketi hiyo baada ya kuwafunga mahasimu wao Misri kwa seti 3-0 katika nusu fainali ya kipute hicho iliyoandaliwa Ijumaa jijini Yaounde,[…]