Uvujaji wa fedha za serikali,Taasisi za Umma zaaswa

Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Prof, Joyce Ndalichako amezionya taasisi mbalimbali za umma zilizochini ya wizara ya elimu kuacha matumizi mabaya ya fedha za serikali ya kulipa posho za kujikimu kinyume na utaratibu. Agizo hilo limetolewa na prof, Joyce Ndalichako wakati akiongea na wakuu wa idara na taasisi za umma zilipo chini ya wizara[…]

Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani, Mkakati wa matumizi ya Kondomu wazinduliwa

Tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI imezindua wiki ya maonesho na huduma kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWi duniani Desemba Mosi pamoja na mkakati wa taifa wa matumizi ya kondomu kwa mwaka 2016 / 2018. Mkakati wa taifa wa matumizi ya kondomu umetayarishwa kueleza vipaumbele vya kimkakati vinavyohitajika kupunguza maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI, magonjwa[…]

Hati Mpya za Ardhi, Kuanza kutolewa mwakani

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi bwana William Lukuvi ameagiza kuanza kutolewa kwa Hati Mpya za Umiliki wa Ardhi ifikapo tarehe moja Mwezi Juni mwakani, ikiwa ni hatua ya kuondoa urasimu na kuongeza ufanisi katika sekta ya ardhi, na kumaliza kabisa migogoro ya ardhi iliyokithiri hapa nchini. Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo jijini[…]

Kuapishwa kwa Rais Kenyatta, Viongozi mataifa zaidi ya 11 kuhudhuria sherehe hizo

Marais 11 kutoka barani Afrika akiwemo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ni miongoni mwa wageni mashuhuri wanaotarajiwa kushuhudia kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta kuhudumu kwa muhula wa pili na wa mwisho hapo kesho jijini Nairobi. Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Kasarani kuanzia saa mbili asubuhi ambapo wizara ya[…]

Papa awasili nchini MYANMAR,Ataka juhudi zaid za kutatua mzozo huo

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis leo anawasili Myanmar akitumai kutia msukumo juhudi za kuutatua mzozo nchini humo ambao umesababisha maelfu ya jamii ya Warohingya, Waislamu walio wachache kuyahama makazi yao kutokana na ghasia na kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh. Kabla ya kupanda ndege kuelekea nchini humo hapo jana, Papa Francis aliwaomba waumini wa[…]

Mkutano wa kupambana na ugaidi,Maafisa kutoka nchi 41 za Kiislam wakutana.

Mwana wa mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameapa kuwaandama magaidi hadi watakapoangamizwa kabisa duniani huku maafisa kutoka nchi 41 za Kiislamu wakikutana kwa mkutano wa kwanza wa nchi zilizo katika muungano wa kijeshi unaopambana dhidi ya ugaidi. Mkutano huo ndiyo wa kwanza wa mawaziri wa ulinzi na maafisa wa ngazi ya juu kutoka[…]