Shambulizi la Kigaidi New York, Watu wanane wamuawa na wengine kadhaa wajeruhiwa

Watu wanane wameuawa mjini New York, Marekani na wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya baada ya dereva wa lori kuwagonga waendesha baiskeli na watembea kwa miguu. Watoto wawili wamejeruhiwa katika tukio hilo ambapo akizungumza na waandishi habari, Meya wa New York, Bill de Blasio amesema kuwa wanalichukulia tukio hilo kama ”shambulizi la kigaidi” na kwamba taarifa zaidi[…]

Hali ya Kisiasa Kenya, Muungano wa mashirika ya kiraia wasema uchaguzi uliofanyika si halali

Muungano wa Mashirika ya kiraia nchini Kenya, umesema matokeo ya Uchaguzi mpya wa urais, sio halali kwa sababu wapiga kura wengi hawakushiriki. Rais wa mashirika hayo Suba Churchil, amesema kuna umuhimu wa kuundwa kwa serikali ya mpito kwa muda wa mwaka mmoja au miwili ili kuandaliwe kwa uchaguzi mwingine, utakaokuwa huru na haki. Hata hivyo,[…]

Hofu ya Mauaji yatikisa Hanang, Kamati ya ulinzi na usalama yaomba wananchi ushirikiano

Watu wawili wameuawa wilayani Hanang katika matukio mawili tofauti likiwemo tukio la ubakaji wa mama mmoja hadi kusababisha kifo chake huku tukio la pili likihusisha mauaji ya Dereva wa Boda boda katika eneo la Basutugan na hadi sasa jeshi la polisi linawashikilia watu tisa kwa kuhusishwa na matukio hayo yanayoambatana wizi wa kuvunja nyumba kwa[…]

Dampo la Pugu kero kwa Wakazi, Wananchi wataka mamlaka husika kuchukua hatua

Mamlaka zinazohusika zimetakiwa kuchukua hatua za haraka kudhibiti maji taka yanayotiririka kutoka kwenye dampo la Pugu Kinyamwezi nje kidogo ya jijini Dar es salaam, ambayo yamefikia hatua ya kupita chini ya ukuta uliozungushwa kwenye dampo hilo hali inayoweza kusababisha madhara kwa jamii inayozunguka eneo hilo. Kamera ya Channel ten imefika katika eneo la Viwege ambalo[…]

Wachina Wanne Mbaroni na Makinikia, Ni wawekezaji wa mgodi ya Zem Tanzania Ltd, Butiama

Jeshi la polis mkoani Mara limefanikiwa kukamata magari mawili aina ya NISSAN PICK UP yaliyobeba masanduku 14 ya mchanga wa madini (MAKINIKIA) wakiwamo raia wanne wa kichina ambao ni wawekezaji wa mgodi wa zem Tanzania Co. L.T.D uliopo Nyasirori wilayani Butiama wakiwa katika harakati za kutorosha mchanga huo wenye uzito wa kilo 700.   Akithibitisha[…]