Watanzania waendelea kujitokeza kununua Tiketi za Fainali za Kombe la Dunia za Russia

Watanzania wameendelea kujitokeza kununua tiketi za Kombe la Dunia zitakazochezwa mwakani nchini Russia. Mpaka sasa kati ya tiketi 290 zilizotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) tiketi za Fainali tayari zimemalizika zikiwa zimebakia tiketi za nusu fainali na hatua ya makundi. Hatua ya makundi ya fainali hizo za Kombe la Dunia ndio yenye[…]

Wananchi wa Musoma Vijijini, Watakiwa kutumia vyanzo vya maji ya ziwa Victoria

Wananchi wa Musoma vijijini mkoani Mara wametakiwa kutumia vyema vyanzo vya maji yanayotokana na ziwa victoria kuendeshea shughuli za kilimo cha umwagiliaji hususani katika zao la Alzet na mahindi ili kujikwamua kiuchumi kuliko kutegemea mvua peke yake. Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo amesema hayo alipokua akizungumza na wananchi wa vijiji vya[…]

Kuelekea Mwaka Mpya wa 2018, Watanzania wakumbushwa kuenzi na kudumisha amani, upendo na umoja

Katika kuelekea mwaka Mpya wa 2018 watanzania wamekumbushwa kuenzi na kudumisha Mshikamano, Amani na Upendo hususani kwa makundi ya wasiojiweza, yatima na wazee kutokana na kwamba, vitendo hivyo vimeendelea kuwa mhimili na kichocheo muhimu katika kufikia Maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Haya yanajidhihirisha kwa vitendo baada ya kikosi cha Jeshi la wananchi 313 Monduli[…]

Matumizi ya Makombora ya Nyuklia, Korea kaskazini yasema haitoacha kama Marekani itaendelea kufanya mazoezi karibu na nchi yake

Korea Kaskazini katika salamu zake za mwisho wa mwaka imesema haitoachana na mpango wake wa silaha za nyuklia ikiwa Marekani na washirika wake wataendelea kufanya mazoezi ya kijeshi karibu na nchi yake. Shirika la habari la Korea Kaskazini limetoa taarifa hiyo leo katika uchambuzi wake kuhusu silaha kubwa za kinyuklia zinazomilikiwa na taifa hilo pamoja[…]

Baada ya Kushinda Uchaguzi Liberia, Rais Mteule George Weah awataka raia wa nchi hiyo wanaoishi ughaibuni kurudi

Rais aliyechaguliwa nchini Liberia George Weah, amewashauri raia wa Liberia wanaoishi nchi za ng’ambo kurudi nyumbani ili kusaidia kuijenga nchi yao. George Weah alitoa wito huo wakati wa mkutano wa kwanza na waandishi wa habari tangu atangazwe kuwa mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika wiki liyopita. Nyota huyo wa zamani wa[…]

Ajali mbaya ya Barabarani Kenya, Yaua watu 36 na wengine zaidi ya 11 kujeruhiwa

Watu 36 wamepoteza maisha na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali mbaya ya barabarani nchini Kenya iliyotokea mapema usiku wa kuamkia leo. Polisi wameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni basi la abiria ambalo lilikuwa linatokea Busia mpani na nchi yaUganda lililokuwa likielekea jijini Nairobi kugongana ana kwa ana lori lililokuwa linatokea mjini Nakuru. Mkuu wa[…]

Msako wa wakwepa Kodi Temeke, Wafanyabiashara wilayani Temeke wapewa siku nne kulipa

Halmashauri ya Manispaa Temeke jijini Dar es salaam imetoa siku nne kuanzia leo Desemba 30 hadi Januari 2 Mwaka 2018 Kwa wafanyabiashara wote wasiolipa kodi na Ushuru mbalimbali kuhakikisha wanalipa katika kipindi hicho ili kuepuka kukumbwa na Operesheni maalum ya Kufunga biashara husika pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria.. Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix[…]

Tamko la rasilimali na Madeni, Viongozi mbalimbali wa Umma wawasilisha fomu zao

Viongozi mbalimbali wa Umma leo wameendelea kufika katika Ofisi za Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma kurejesha tamko la rasilimali na madeni yao kama wanavyotakiwa kisheria kabla ya siku ya mwisho Desemba 31, 2017. Mwitikio huo unafuatia sekretariati hiyo kutoa tamko kuwa ofisi zake katika kanda zote zitaendelea kuwa wazi siku ya jumamosi Desemba[…]

PM amekwishawasilisha tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema amekwishawasilisha tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma tangu jana Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake Namahema ‘A’ wilayani Ruangwa mkoani Lindi Waziri Mkuu amesema fomu hizo zilipokelewa jana na amekwishapatiwa barua ya kupokea tamko hilo. Aidha waziri mkuu[…]