TRUMP AHUTUBIA BARAZA LA CONGRESS,Awatolewa wito Wamarekani kuweka pembeni tofauti zao

Saa chache baada ya Rais Donald Trump,kuhutubia Taifa hilo kwa mara ya kwanza,seneta Berni Sanders,ameikosoa hotuba ya Rais huyo kwa madai kuwa haikugusa maeneo kadhaa ikiwemo pengo kati ya matajiri na masikini,masuala ya hali ya hewa ikiwamo vitisho vya msingi dhidi ya nchi hiyo. Katika sehemu ya hotuba yake, Rais Trump, kutoka chama cha Republican,[…]

Sakata la ODINGA Kujiapisha,Baadhi wadai amewafurahisha wafuasi wake

Watu mbalimbali nchini Kenya,wametoa maoni yao kufuatia kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, kujiapisha kuwa rais wa watu. Miongoni mwa waliotoa maoni yao kuhusina na tukio hilo la jana,ni wasomi,wachambuzi wa siasa za kenya na wananchi. Mmoja wa wasomi nchini humo,amesema,kitendo alichofanya bwana Odinga,hakina maana zaidi ya kuwafurahisha na kuwatuliza wafuasi wake,kwakuwa sherehe[…]

Hati za kusafiria za KIELEKTRONIKA,Tanzania yatumia Shilingi Bilion 127.2 kufanikisha mradi

Serikali imezindua hati za kusafiria za kielektroniki za Afrika mashariki za Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa Makubaliano ya wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kutaka kila raia wa nchi hizo kutumia hati hizo. Mradi wa kutengeneza Hati za kusafiria za Kielektronika maarufu kama Passports, umefadhiliwa na serikali ya Tanzania kwa gharama[…]

Machafuko CONGO DRC,UNHCR ladai wakimbizi 1,200 wakimbilia Tz

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi la UNHCR, limedai kuwa jumla ya wakimbizi 1200,raia wa jamhuri ya Demokrasia ya Congo,wameyakimbia mapigano yanayoendelea Mashariki mwa nchi hiyo na kuingia Tanzania. Aidha shirika hilo limedai Maelfu ya watoto, wanawake na wanaume, wameacha makazi yao kukimbia mapigano dhidi ya makundi yenye silaha ya Mai Mai yanayoendelea Kusini[…]

Kuapishwa kwa RAILA ODINGA Kenya,Mamia ya watu walijitokeza katika viwanja vya UHURU jijini NAIROBI

Mamia ya watu walijitokeza katika viwanja vya UHURU jijini NAIROBI ili kushuhudia kuapishwa kwa RAILA ODINGA,ambae ni kiongozi wa muungano wa NASA,anaejinasibu kwamba alishinda uchaguzi mwezi wa oktoba mwaka jana wamepigwa na butwaa badaa ya kiongozi huyo kutumia muda mfupi viwanjani hapo kwani baada ya kula kiapo aliondoka huku akisema kuapa huko sio mapinduzi ya[…]

Viwanda vya kuchakata samaki,Serikali yaagiza vifunguliwe ifikapo Julai Mosi mwaka huu

Waziri wa Mifugo na Uvuvi LUHAGA MPINA amewaagiza wamiliki wote wa Viwanda vya kuchakata samaki vilivyopo kanda ya ziwa Victoria kuanza kazi ifikapo Julai mosi mwaka huu huku akiwataka kuwasilisha mpango kazi wa viwanda hivyo wizarani kwake kabla ya mwezi Machi mwaka huu. Akizungumza katika zoezi la kuchoma zana za uvuvi haramu waziri mpina amewataka[…]

Umeme Barani Afrika,Nchi za Afrika zaazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa nishati hiyo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuchochea kasi ya maendeleo. Waziri Mkuu ameyasema hayo jana Januari 29 alipozungumza baada ya mkutano wa Viongozi na Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia ambapo alimuwakilisha Rais Dk. John Magufuli Amesema[…]

Matokeo ya mtihani wa kidato cha NNE 2017,Baraza la Mitihani lasema kiwango cha ufaulu kimeongezeka

Baraza la mitihani Tanzania NECTA limesema mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana kuanzia oktaba hadi novemba ulighubikwa na baadhi ya vitendo vya udanganyifu ambapo jumla ya watahiniwa 265 wamebainika kufanya udanganyifu wa aina mbalimbali ikiwemo kukamatwa na vitu visivyofaa kuingia navyo katika chumba cha mtihani pamoja na watahiniwa kufanyiwa mtihani wa watu wengine.[…]