Korea Kaskazini,Yadaiwa kupeleka silaha za Kemikali Syria

Jopo la wataalamu wanaofuatailia vikwazo dhidi ya Korea kaskazini, limedai kuwa Korea Kusini,ilipeleka nchini Syria vifaa vinavyowea kutumika kutengeneza makombora na silaha za kemikali. Kwa mujibu wa jopo hilo,nchi hiyo pia imepeleka wataalamu wa kutengeza makombora na kukiuka vikwazo vya Umoja wa mataifa. Aidha imedaiwa pia kupeleka mifumo ya makombora yaliyopigwa marufuku nchini Myanamar. Share[…]

Suala la Uingereza Kujitoa Umoja wa Ulaya- EU,Kuwasilishwa kwa Rasimu ya Brexit huenda kukaleta mvutano

Mjumbe kiongozi wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo ya Uingereza kujiondoa katika umoja huo marufu kama Brexit,Mishel Bania,alikuwa anatarajiwa kutangaza rasimu ya Brexit,iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu. Rasimu hiyo inatishia kuleta mvutano mpya na Uingereza kuhusu masuala muhimu kufutiatia waraka huo kuonekana kutozingatia matakwa ya Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May,kuhusu mpka na Ireland,haki za[…]

Mapamabano dhidi ya Boko Haram -Nigeria,Raia 1,130 wakombolewa, wafuasi wa kundi hilo 37 wauawa

Takriban raia 1,130 wamekombolewa na washukiwa 37 wa kundi la wanamgambo wa Boko Haram,wameuwa katika mashambulizi yaliyotekelezwa kwa pamoja na vikosi vya majeshi ya Cameroon na Nigeria,kuzunguka jimbo la ziwa Chad. Taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi la Nigeria,kanali Onyema Nwackukwu,operesheni hiyo imefanyika katika mpaka wa vijiji vya Kusha-Kucha, Surdewala, Alkanerik, Magdewerne na Mayen na[…]

Taarifa ya makisio ya idadi ya watu,Tanzania yakadiriwa kuwa watu mil. 61.2 kufikia mwaka 2022

Tanzania imezindua taarifa ya makisio ya idadi ya watu kwa mwaka 2013-2035 ambayo inaonyesha kufikia mwaka 2022 Tanzania inakadiriwa itakuwa na watu wapatao milioni 61.2 ikiwa ni ongezeko la watu milioni 16.3 tangu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 iliyoonyesha idadi ya watu kuwa milioni 44.9 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa taarifa hiyo,[…]

Malalamiko ya wachimbaji wadogo,Wampokea Naibu Waziri wa Madini wakiwa na mabango

  Naibu Waziri wa Madini Stansalaus Nyongo aliyekuwa ziarani Mkoani Geita, kikazi amemaliza ziara hiyo kwa kupokewa na mabango na wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Jikomboe katika Kijiji cha Msasa Wilayani Chato, Mkoani humo. Mambango hayo yaliyokuwa yamebebwa na baadhi ya wachimbaji katika Mgodi huo, yalisomeka kuwa baadhi wamiliki wa leseni za uchimbaji wamekuwa wakiwanyanyasa[…]

Watoto wenye uhitaji maalum,Wazazi na walezi watakiwa kutowakosesha haki ya kupata elimu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wazazi na walezi wa watoto wenye uhitaji maalumu kutowafungia ndani na badala yake wawapeleke shule kwani amesema si kigezo cha kuwakosesha watoto hao kupata elimu na kufanya kazi Ametoa rai hiyo wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa majengo ya chuo cha Ualimu Kitangali, kilichopo Newala mkoani Mtwara ambapo ametahadharisha kuwa[…]

Ukatili na mauaji Zimbabwe miaka 30 iliyopita,Kamisheni ya Amani na Maridhiano yaanza kusikiliza tuhuma

  Katika shauri hilo la wazi,imedaiwa kuwa rais huyo wa zamani wa Zimbabwe,aliamuru kuuawa kwa watu katika jimbo la Matebele,alioamini kuwa walikuwa wanajaribu kumuondoa madarakani. Hata hivyo wengi wanahisi kuwa shauri hilo linalosikilizwa na Kamisheni hiyo,ni kupoteza muda kwakuwa imewekwa na serikali. Imeelezwa kuwa wakati wa mauaji hayo,yaliyogharimu maelfu ya wananchi wa eneo hilo,Rais wa[…]

Mabadiliko ya baraza la Mawaziri,Waliofutwa kazi na Zuma warejeshwa kazini

Rais mpya wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemteua Nhlanhla Nene kuwa waziri wa fedha , miaka miwili baada ya kufukuzwa kwake katika nafasi hiyo kulivyosababisha uasi ndani ya chama tawala ambao hatimaye umemuondoa kiongozi wa zamani Jacob Zuma. Mabadiliko hayo ya baraza la mawaziri pia yameshuhudia rais Ramaphosa akiingiza sura mpya na kuwaondoa baadhi ya[…]

Umoja wa mataifa na walinda amani,Wawarejesha nyumbani waliohusika na unyanyasaji wa kingono

Umoja wa mataifa umesema umewaita nyumbani walinda amani 46 kutoka Ghana waliotuhumiwa kufanya unyanyasaji wa kingono wakati wa shughuli zao nchini Sudan Kusini. Msemaji wa umoja wa mataifa amesema kulikuwa na taarifa za walinda amani wa Ghana kutuhumiwa kununua wanawake kwa ajili ya kufanya ngono. Amesema umoja wa mataifa hautafumbia macho tabia kama hizo nchini[…]

Usalama wa Rais Syria,Russia yataka usitishwaji mapigano

Rais wa Urusi Vladmir Putin ameagiza usitishwaji wa mapigano kwa takriban saa tano katika mashambulizi yanayofanywa na serikali ya Syria katika maeneo ya mashariki mwa eneo la Ghouta linalodhibitiwa na waasi. Usitishwaji huo wa mapigano unaanza leo Jumanne na utajumuisha kuundwa kwa kile kinachoitwa ” Njia ya Hisani” kuwawezesha raia kuondoka katika eneo hilo lenye[…]