Changamoto ya usafiri Bonde la Ziwa RUKWA,Wananchi wameiomba serikali kuboresha miundombinu ya barabara inayounganisha vijiji hivyo

Baadhi ya wananchi wanaoishi katika vijiji 39 vilivyopo Bonde la Ziwa RUKWA katika halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wameiomba serikali kuboresha miundombinu ya barabara inayounganisha vijiji hivyo. Baadhi ya wananchi hao wanaojihusisha na kilimo cha mpunga na mazao mengine ya nafaka pamoja na uvuvi wanakabiliwa na changamoto ya usafirishaji wa mazao yao kutokana[…]

Mgomo wa madaktari Drc congo,Waairishwa baada ya serikali kukubali kuutafutia ufumbuzi

Kamati ya kitaifa inayotetea maslahi ya madaktari wa DRCongo (SYMECO) imetangaza kuwa mgomo uliokuwa umepangwa kufanyika Jumatatu hii Aprili 30 nchi nzima hautafanyika tena. Mkuu wa Kamati hiyo Juvenal Muanda Nlenda, amesema serikali imekubali kujibu madai yao, ambayo ni ongezeko la mshara kwa asilimia 100 miongoni mwa madai mengine. Madaktari nchini DR Congo walikua wanaomba[…]

Makubaliano ya mkataba wa silaha za nyuklia wa Iran,Uingereza, Urafansa na Ujerumani waaahidi kuunga mkono

Viongozi wa Uingereza , Ufaransa na Ujerumani wameahidi kuunga mkono makubaliano ya sasa ya nyukilia yaliyofikiwa mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa makubwa yenye nguvu duniani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza viongozi wa nchi hizo tatu wamesema makubaliano hayo ni njia nzuri inayosaidia kupunguza kitisho cha silaha[…]

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Simiyu,Baada ya Daraja la Mto Nyanza kutitia na baadhi ya kingo kuwa na nyufa kubwa

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Simiyu, zimeleta adha kwa wananchi mkoani humo na kusababisha baadhi ya Wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo, wilayani Meatu baada ya Daraja la Mto Nyanza lililopo wilayani humo, kutitia na baadhi ya kingo kuwa na nyufa kubwa na kusababisha kukatika kwa mawasiliano kwa Wanachi wa Kata za Mwandoya na Mwakisandu. Wakizungumza na[…]

Mpango wa kudhibiti dawa bandia Afrika,Wawakilishi wa nchi za Afrika wakutana Dar es Salaam

Tanzania na nchi nyingine za Afrika zimefikia makubaliano ya kushirikiana katika kufuatilia matumizi ya dawa za binadamu ili kuhakikisha kwamba dawa bandia hazipenyi katika mfumo wa matumizi, hatua inayoweza kuathiri mfumo wa matibabu. Akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya tiba kutoka nchi tisa za Afrika na Ulaya, unaofanyika jijini Dar es Salaam kupanga mkakati[…]

Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,kupokelewa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ulungu kulalamikia ukosefu wa vyoo shuleni kwao

Baadhi ya shule za msingi katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa zimefungwa kwa kukosa vyoo ambapo inadaiwa zitafunguliwa kuendelea na masomo baada ya ujenzi wa vyoo kukamilika katika shule hizo. Hayo yamebainika wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege Sinkamba katika kijiji cha Tatanda Kata ya Sopa wilaya ya Kalambo[…]

Uzinduzi kiwanda cha kutengeza mita za luku nchini,Waziri Kalemani amesema ili kuifanya Tanesco iweze kutoa huduma bora

Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani ameitaja sababu ya gharama kubwa za uendeshaji wa shirika la Umeme Tanzania Tanesco ndiyo inayolifanya shirika hilo kushindwa kufanya vizuri na kusababisha kushindwa kutoa huduma bora kwa wateja wake. Gharama hizo kubwa zinatokana na shirika hilo kuagiza vifaa mbalimbali nje ya nchi ikiwemo Nguzo za umeme ambazo zilikuwa zikitoka[…]

Hatua ya kufunga majaribio ya silaha za nyuklia,Rais wa korea kaskazini na kusini wakubaliana nchi zao kutorudi katika vita

Korea Kaskazini imeapa kulifunga eneo lililotumika kwa majaribio ya silaha za nyuklia la Punggye-ri mapema mwezi ujao. Kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Korea Kusini, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in wamekubaliana kutangaza azma hiyo hadharani, wakati Korea Kaskazini itakapokuwa ikiharibu eneo hilo mnamo mwezi Mei,[…]