Dodoma – Hati za Kimila za Umiliki wa Ardhi zatolewa

Jumla ya vijiji 107 wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma vipo katika mpango wa kunufaika na hati za kimila za umiliki wa rasilimali ardhi chini ya Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA). Akizungumza katika zoezi la ugawaji wa hati za kimila 30 kwa wananchi wa vijiji vya Membe na Mahama wilayani hapa[…]

Wanafunzi wanne wamefariki kwa kuzama kwenye mwambao wa bahari ya hindi wakiwa kwenye hafla ya kusheherekea matokeo yao ya mtihani

Wanafunzi wanne wa Shule ya Sekondari Kimbiji iliyopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wamepoteza maisha baada ya kuzama kwenye mwambao wa bahari ya hindi wakati wakiwa kwenye hafla ya kusheherekea matokeo yao ya mtihani wa Mocko wa kidato cha nne ambapo shule hiyo imeshika nafasi ya kumi kwa mkoa wa Dar es Salaam[…]

Rais wa Marekani Trump amesema hana tatizo lolote kukutana na viongozi wa Iran wakati wowote

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hana tatizo lolote kukutana na viongozi wa Iran wakati wowote wanaotaka kufanya mikutano hiyo bila kuwekwa masharti yoyote. Hata hivyo, Rais huyo wa Marekani amesema uongozi wa Iran unaunga mkono magaidi ambao lazima wazuiwe kumiliki silaha za nyuklia. Matamshi ya Trump yanafuatia siku kadhaa za majibizano makali kati ya[…]

Mita Mpya za Maji zazinduliwa

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa ametoa miezi miwili kwa wakazi wa jiji la dar es Salaam  waliojiunganishia maji kwa ujanja ujanja kujisalimisha shirika la maji safi na maji taka dar es salaam – Dawasco ili watambulike na kuhalalishiwa huduma hiyo lakini ameonya kuwachukulia hatua za kisheria wezi wakubwa wa maji. **Prof.Mbarawa ametoa rai[…]

Tambani Mkuranga waomba kujengewa kituo cha Polisi

Wananchi wa Kitongoji cha Tambani ëAí kilichopo katika Kijiji cha Tambani, Kata ya Tambani Wilayani Mkuranga wameuomba uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha kituo cha Polisi cha Kata ya Tambani kinajengwa ili kudhibiti matukio  ya uhalifu ya uvamizi kwa kutumia silaha Kauli hiyo imetolewa na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kitongoji hicho kuwa wanaomba kituo[…]

Serikali Imedhamiria kuinua kilimo Nchini

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali imedhamiria kuinua na kuboresha shughuli za kilimo kwa kuwasaidia wakulima kupata mbegu bora madawa na masoko ya uhakika jambo litakalochangia uchumi wa nchi kukua kwa kasi katika kuelekea uchumi wa kati ifikapo 2025. Kauli hiyo imetolewa wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyarubanda wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma[…]

Makamu wa Rais atasimamia mgawanyo wa Maji katika mto Ruaha Mkuu ili kuwe na usawa wa matumizi

MAKAMU wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, amesema yuko tayari kusimamia mgawanyo wa  maji kutoka Mto Ruaha Mkuu, kwa kuzingatia usawa wa matumizi kati ya serikali, wakulima, wafugaji na kwa ajili ya wanyama katika hifadhi ya taifa ya Ruaha. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan anasema haya kwenye mkutano wa hadhara wakati akihutubia wananchi, […]

China haina haja ya kudhibiti kiwango cha ubadilishaji wa sarafu yake RMB

Marekani hivi karibuni imeishutumu China kudhibiti kiwango cha ubadilishaji wa sarafu yake ya RMB. Mchumi mkuu wa Shirika la Fedha Duniani IMF Bw. Maurice Obstfeld amesema hakuna ushahidi unaoweza kuthibitisha shutuma hiyo. “China kudhibiti kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya RMB” ni kisingizio kinachotumiwa na Marekani mara kwa mara. Ukweli ni kwamba kiwango hicho kinaamuliwa[…]