Tanzania na Korea ya Kusini zimesaini makubaliano mapya ya mkataba wa kidiplomasia

Tanzania na Korea ya Kusini zimesaini makubaliano mapya ya mkataba wa kidiplomasia wa hati ya kusafiria ambayo pia inaondoa zuio la Visa kwa Raia wote wa nchi hizo mbili wanaosafiri kwa shughuli za kidiplomasia na kiutumishi, lengo likiwa kumarisha uhusiano wa nchi hizo mbili. Akizungumza baada ya zoezi la utiaji saini wa makubaliano hayo, lililofanyika[…]

Wakulima watakiwa kuunda vikundi

Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba amewataka wakulima nchini kuunda vikundi vya umoja vya ushirika ili kupata bei nzuri pindi wanapotaka kuuza Mazao yao. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya wakulima yanayofanyika katka kituo cha utafiti wa kilimo cha Selian mkoani Arusha Dr Charles Tizeba  amesema kuwa kupitia  ushirika wao  serikali pia itakuwa na[…]

Wamachinga wafanya usafi Gerezani

Wafanyabiashara wadogo Maarufu kama Wamachinga leo wameendesha zoezi la Usafi katika eneo Kituo cha mabasi cha Mwendokasi Kariakoo Gerezani ikiwa ni kuunga Mkono Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda la kutaka wafanyabiashara wote kuhakikisha maeneo yao ya biashara yanakuwa masafi wakati wote kabla ya Kuanza kusimamiwa na vijana wa JKT na Mgambo.[…]

Wawekezaji kwenye mashamba ya ngano wilaya ya hanang wameiomba serikali kudhibiti uingizwaji wa zao kutoka nje

Wawekezaji kwenye mashamba ya ngano wilaya ya hanang wameiomba serikali kudhibiti uingizwaji wa zao kutoka nje ili kusaidia wazalishaji wa ndani kupata soko kwa urahisi na kuepuka kuharibika kwa ngano kutokana na kukaa mda mrefu kwenye maghala huku pia wakiomba uwazi katika uwekezaji wa kilimo. Rilasha kailiya mkurugenzi wa kampuni ya ngano limited inayomiliki mashamba[…]

UUZWAJI HOLELA DAWA ZA KILIMO SONGEA

Wakulima wa korosho na wadau wa pembejeo za kilimo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuzuia uuzwaji holela wa madawa ya kilimo pamoja na ingizwaji wa madawa hayo kutoka nje ya nchi yaliyoandikwa kwa Lugha ya Kireno,baadhi ya dawa wanapopuliza haina uwezo wa kuua wadudu na inakausha mikorosho. Share on: WhatsApp

Waziri wa Maliasili na utalii aagiza wataalam wa mazingiza kutathmini jambo hili

Waziri  wa maliasili na utalii Dkt. Hamis Kigwangallah ameiagiza halmashauri ya wilaya ya sikonge kupeleka wataalam wa masuala ya mazingira ili wafanye tathmini juu ya athari za kimazingira zinazoweza kujitokeza katika skim ya umwagiliaji ya ulua ambayo imejengwa ndani ya hifadhi ya msitu wa ipembamipasi iliyopo wilayani sikonge mkoani Tabora. Share on: WhatsApp