Uzinduzi kampeni za uchaguzi mdogo wa wabunge zimezinduliwa rasmi ambapo mchuano mkali kwa hatua za awali ukionekana Kati ya CCM na CHADEMA

Kampeni za uchaguzi mdogo wa wabunge zimezinduliwa rasmi jana wilayani Monduli mkoani ambapo mchuano mkali kwa hatua za awali ukionekana Kati ya chama cha mapinduzi CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA . Uchaguzi huu unafuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chadema Julius Kalanga kujiuzulu nafasi hiyo na kukihama chama hicho na kujiunga[…]

Rais Magufuli amewataka viongozi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria sambamba na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi ya wananchi.

Rais ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa wilaya hiyo, ambapo amesisitiza kuwa viongozi wote wajenge utaratibu wa kusoma sheria na kujiepusha kutumiwa kwa maslahi ya watu binafsi. Akitolea mfano wa mgogoro wa makontena yanayodaiwa kuwa na fenicha za shule, na yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika bandari ya Dar[…]

Wizara ya mifugo na uvuvi imesema kukosekana kwa mawasiliano mazuri baina ya wizara na watumishi yamesababisha kushindwa kuchangia utoaji wa huduma za kijamii na mapato serikali

Katibu Mkuu wizara ya mifugo na uvuvi Dk.Rashid Tamatahah amesema kuwa wizara yake inakabiliwa na changamoto ya kushindwa kuchangia utoaji wa huduma za kijamii na mapato serikali kutokana na usimamizi dhaifu wa sheria na kukosekana kwa mawasiliano mazuri baina ya wizara na watumishi wake katika halmashauri mbalimbali nchini. Katibu mkuu wizara hiyo ya mifugo na[…]

Baada ya kuzindua Mkakati wa Unywaji Dawa kwa wanafunzi kuanzia miaka 5-hadi 14 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema dawa hizo ni salama na hazina madhara kwa watoto

Wazazi na walezi mkoani Dar es Salaam wamehamasishwa kuhakikisha watoto wao wanaoanzia Umri wa miaka 5 hadi 14 wanakunywa Dawa za kinga dhidi ya magonjwa ya kichocho pamoja na minyoo ili kujikinga na magonjwa hayo hatari kwa watoto. Akizungumza baada ya kuzindua Mkakati wa Unywaji Dawa kwa wanafunzi kuanzia miaka 5-hadi 14 Mkuu wa Mkoa[…]

Mkoa wa kigoma wachukua tahadhari na hatua za kuzuia maambuzi ya ugonjwa wa Ebola kwa kutoa elimu ya namna ya kujikinga

Mkoa wa kigoma umeanza kuchukua tahadhari na hatua za kuzuia maambuzi ya ugonjwa wa Ebola kwa kutoa elimu ya namna ya kujikinga kupitia taasisi za kidini pamoja na waganga wajadi kutokana na mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa yenye hatari kubwa ya kuingia na kuenea kwa ugonjwa huo. Akitoa taarifa kuhusu ugonjwa huo Mganga mkuu[…]

Serikali yazionya taasisi za kibenki kusimamia na kukomesha udokozi wa fedha za wateja unaofanywa na baadhi ya watumishi wao

Serikali imezionya benki zote nchini, kusimamia na kukomesha udokozi wa fedha za wateja, unaofanywa na baadhi ya watumishi wao, na wakishindwa kufanya hivyo, serikali haitasita kuchukua hatua kali, ikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni zao za uendeshaji. Onyo hilo limetolewa jijini Dodoma na Naibu waziri wa fedha na mipango, Dk. Ashantu Kijaji, wakati alipokuwa akifungua[…]

Serikali kumaliza tatizo la uhaba wa vifaranga na kuruhusu kuingizwa kwa mayai kutoka nje ya nchi

Serikali imewatoa hofu wafugaji wa kuku nchini kuwa, imeshachukua hatua thabiti za kuondoa uhaba wa vifaranga kwa kuruhusu kuingizwa nchini kwa mayai ya kuzalisha vifaranga, huku kampuni za ndani zikijengewa pia uwezo wa kutosheleza mahitaji ya soko. Uhakikisho huo wa serikali umetolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw. Abdallah Ulega, wakati[…]