Serikali ya Tanzania imetiliana saini na Kampuni tano za ukandarasi za Serikali ya Korea ya Kusini ya mkataba wa ujenzi wa meli mpya ya kisasa pamoja na ukarabati wa meli tatu

Tatizo la ukosefu wa usafiri wa uhakika katika Ziwa Victoria linatarajia kutoweka, baada ya Serikali ya Tanzania kutiliana saini na Kampuni tano za ukandarasi za Serikali ya Korea ya Kusini ya mkataba wa ujenzi wa meli mpya ya kisasa pamoja na ukarabati wa meli tatu. Mkataba huo wa shilingi Billioni 152 utahusisha ujenzi wa meli[…]

China yafanya juhudi kujenga Jumuiya yenye hatma ya pamoja iliyo karibu zaidi kati yake na Afrika

Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika ulioanza leo hapa Beijing. Katika hotuba hiyo, rais Xi amesema katika miaka mitatu ijayo na kipindi kifuatacho, China itajenga Jumuiya yenye hatma ya pamoja kati yake na Afrika iliyo ya karibu zaidi kwa njia ya[…]

Mkutano wa mwaka 2018 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wafunguliwa Beijing

Mkutano wa mwaka 2018 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umefunguliwa leo hapa Beijing, ambapo rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwenye mkutano huo. Amesisitiza kuwa, China inapenda kushirikiana na Afrika kujenga jumuiya yenye mutakabali wa pamoja inayobeba majukumu kwa pamoja, kufanya ushirikiano wa kunufaishana, kusitawisha pamoja tamaduni, kujenga[…]

LIONS CLUB yazindua mkakati wa kutunza mazingira nakufanya usafi katika fukwe za bahari ya hindi

Wanachama wa LIONS CLUB wamezindua mkakati wa kutunza mazingira kwa kuonyesha jamii njia sahihi ya kuyatunza ambapo wameiwezesha kwa na vifaa vya kutunzia taka za aina tofauti. Akizungumza katika uzinduzi huo ambao ulifanywa sambamba na kusafisha mazingira katika fukwe za bahari ya Hindi karibu na eneo la hospitali ya Aghakan mwakilishi wa shirika la umoja[…]

Kufuatia mapigano yanayoendelea nchini Libya,Zaidi ya wafungwa 400 watoroka kutoka katika jela.

Hali ya hatari imetangazwa mjini Tripoli na maeneo yaliyo karibu na mji huo kufuatia mapigano makali kati ya makundi hasimu ya wapiganaji ambayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 39 na wengine kadhaa kujeruhiwa. Serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa kutokana na hatari iliyopo kufuatia mapigano hayo na kuzingatia na maslahi ya[…]

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza kukamatwa Mkandarasi aliyejenga daraja la kijiji cha Nyanza, wilayani Meatu, Mkoani Simiyu.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza kukamatwa Mkandarasi aliyejenga daraja la kijiji cha Nyanza, wilayani Meatu, Mkoani Simiyu, lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 lililojengwa chini ya kiwango na kusababisha kubomoka ndani ya miezi minne tangu kukamilika ujenzi wake huku akiwatupia lawama viongozi wa wilaya hiyo kwa kushindwa kusimamia miradi ya[…]

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde ameyataka makampuni nchini kuweka utaratibu wa kutoa ajira kwa wahitimu

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde ameyataka makampuni nchini kuweka utaratibu wa kutoa ajira kwa wahitimu wanaotoka moja kwa moja vyuoni, badala ya utaratibu uliozoeleka wa kuwapa ajira wale wenye uzoefu pekee. Akizungumza katika hafla ya kufungua kituo maalumu cha mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi wapya na wale waliopo[…]