Marekani kuzidisha vita ya biashara na China hakutasaidia utatuzi wa suala

Marekani imetangaza kuongeza ushuru wa forodha kwa asilimia 10 kwa bidhaa kutoka China zenye thamani ya dola bilioni 200 za kimarekani kuanzia tarehe 24, na kutishia kuchukua hatua zaidi dhidi ya China. Wizara ya biashara ya China imeeleza masikitiko makubwa, na kusema China itajibu hatua hiyo ya Marekani kwa wakati mmoja. Wachambuzi wanaona kuwa bila[…]

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amezuru jijini Pyongyang nchini Korea Kaskazini ambako amekutana na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un.

Ziara ya Moon inalenga kuendeleza mazungumzo na serikali ya Korea Kaskazini kuhusu kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia na kuimarisha uhusiano wake na Marekani. Baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Kim Jong UN, rais Moon alitembezwa katikati ya jiji la Pyongyang na kusalimiwa[…]

Mataifa mawili yakutana kujadili hatma ya vita vya Syria katika kulikomboa jimbo la Idlib

Rais Vladimir Putin pamoja na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki wamekutana kujadili hatima ya vita vya Syria kuelekea kulikomboa jimbo la Idlib ambalo ndio la mwisho linalodhibitiwa na waasi. Uturuki imekuwa ikijaribu kuzuia kufanyika operesheni kubwa ya kijeshi katika jimbo hilo la Idlib, ambalo lipo karibu na mpaka wake. Vikosi vya serikali ya Syria[…]

Idara ya Uhamiaji mkoa wa Mara yafanikiwa kukamata wahamiaji haramu sita kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria

Katika kuhakiksha kunakuwepo na udhibiti wa vitendo vya uhalifu ikiwemo biashara haramu ya uuzaji wa binadamu hususan katika maeneo mengi ya mpakani, Idara ya uhamiaji mkoani Mara imefanikiwa kuwakamata watu sita raia wa nchini Ethiopia na Somalia, kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria kwa kupitia njia za panya. Akizungumza na waandishi wa habari[…]

Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania ameuagiza uongozi wa Chama Cha Ushirika Cha Wafugaji wa Njombe kufanya uchaguzi wa viongozi wapya

Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dokta TITUS KAMANI ameuagiza uongozi wa Chama Cha Ushirika Cha Wafugaji wa Njombe (NJOLIFA LTD) kufanya uchaguzi wa viongozi wapya, baada ya kutoridhishwa na hali ya utendaji wa ushirika huo ambao umedumu madarakani kwa zaidi ya miaka sita sasa , bila kuleta tija kwa wafugaji mkoani Njombe.[…]

Wakala wa barabara Mkoa wa Dodoma (TARURA) wameanza zoezi la ufungaji taa za barabarani katika mkoa huo

Wakala wa barabara Mkoa wa Dodoma (TARURA) wameanza zoezi la kufunga taa kwenye barabara ya kutokea kwa Waziri Mkuu ili kuifanya barabara hiyo kuwa na mwanga na kusaidia kudhibiti uhalifu unaotokana na kuwepo kwa giza. Akizungumza wakati wa zoezi hilo la uwekaji wa taa za mionzi jua (SOLAR), Meneja wa TARURA mkoa wa Dodoma Eng.[…]