Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar, hatimaye amerejea mjini Juba baada ya miaka miwili akiwa uhamishoni, ikiwa ni maandalizi ya sherehe ya kutiliwa saini ya mkataba wa amani mwezi Septemba

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar, hatimaye amerejea mjini Juba baada ya miaka miwili akiwa uhamishoni, ikiwa ni maandalizi ya sherehe ya kutiliwa saini ya mkataba wa amani mwezi Septemba, licha ya wasiwasi kuhusu usalama wake. Mmoja wa wasemaji wake Lam Paul Gabriel amesema Bw Machar, kiongozi wa wa kundi la waasi la[…]

Kampuni ya GSM Tanzania imetangaza uwekezaji kwenye sekta ya kilimo kwa kuzalisha mboleo ya kukuzia mazao, ambayo itapatikana kupitia kampuni yake tanzu ya GS Agro.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni hiyo Matina Nkurlu amewaambia waandishi wa habari waliotembelea maghala ya kuhifadhi mbolea hiyo jijini Dar es Salaam kwamba uwekezaji huo umelenga kuunga mkono uzalishaji kupitia kilimo. Amesema kwa kutambua kwamba zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanategemea kilimo kukuza uchumi wao, GSM imeona ni vema kukidhi mahitaji ya pembejeo,[…]

Serikali imeahidi kuharakisha juhudi za kuondoa changamoto zinazo wakabili wawekezaji wa kiwanda cha saruji cha Hangya kinachojengwa wilayani mkinga mkoani Tanga ili kiweze kukamilika na kuanza kazi mara moja.

Kauli hiyo imetolewa na waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa viwanda vya kampuni ya SINOMA Hangya ya china katika ziara yake mkoani Hapa. Amesema sera ya Serikali ya awamu ya tano ni kuimarisha uchumi wa viwanda kwa kujenga mazingira bora yatakayovutia wawekezaji kuja nchini na kutoa ajira kwa wananchi. Akihutubia wananchi[…]

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na majeshi ya ulinzi na usalama wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki limepanga kufanya mafunzo ya kijeshi kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kiutendaji

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na majeshi ya ulinzi na usalama wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki limepanga kufanya mafunzo ya kijeshi kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kiutendaji na kuimarisha uhusiano wa nchi hizo. Mafunzo hayo yanatarajiwa kufuguliwa rasmi Novemba 5 na kufikia tamati Novemba 21 mwaka huu mkoani Tanga[…]

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda ameunda kamati ya Uchunguzi ya watu 18 kuchunguza matukio ya Vitendo vya Ukiukwaji wa maadili ikiwemo Vitendo vya Ushoga, Usagaji pamoja Uchangudoa

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda ameunda kamati ya Uchunguzi ya watu 18 kuchunguza matukio ya Vitendo vya Ukiukwaji wa maadili ikiwemo Vitendo vya Ushoga, Usagaji pamoja Uchangudoa ambavyo vimeonekana kushika kasi kwa kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dsm Makonda amesema Kumekuwapo na Ukiukwaji wa Maadili na Utamaduni[…]

Vibarua 45 wanaofanya kazi katika Bohari Kuu ya Madawa MSD upande wa kupakua na kupakia madawa jijini Dar es salaam wameiomba Serikali iwasaidie kupata stahiki zao za mishahara pamoja na kiinua mgongo baada ya kupewa notisi ya kusitisha mkataba wa kazi

Vibarua 45 wanaofanya kazi katika Bohari Kuu ya Madawa MSD upande wa kupakua na kupakia madawa jijini Dar es salaam wameiomba Serikali iwasaidie kupata stahiki zao za mishahara pamoja na kiinua mgongo baada ya kupewa notisi ya kusitisha mkataba wa kazi bila ya kupewa stahiki zao mihimu. Wakizungumza na Channel Ten jijini Dar es salaam[…]

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limepitisha kwa kauli moja azimio linalotaka kuimarisha zaidi uwezo katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23, Umoja wa Mataifa umeyataka makundi ya watu wenye silaha kusitisha mapambano ili kuruhusu misaada ya kibinadamu na huduma za kiafya kuwafikia raia katika maeneo yanayoathiriwa na ugonjwa wa Ebola. Azimio hilo pia linasisitiza haja ya MONUSCO na shirika la Afya Duniani (WHO) kuratibu shughuli hizo[…]

Mchumba wa mwandishi habari aliyeuwawa Jamal Khashoggi Hatice Cengiz amemtaka Rais Donald Trump na viongozi wengine kuhakikisha kwamba taarifa za kifo chake katika ubalozi mdogo wa Uturuki mjini Istanbul hazitafichwa.

Waendesha mashitaka wa Saudi Arabia na Uturuki wamekutana kwa siku ya pili kujadili juu ya uchunguzi wa kifo hicho. Akizungumza katika kumbukumbu mjini London Hatice Cengiz ameeleza kuvunjika kwake moyo na uongozi wa nchi nyingi. Akimtaja Rais Trump, amemtaka kusaidia kufichua ukweli na kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake. Cengiz pia ameuambia mkusanyiko huo wa kumbukumbu[…]

Vikosi vya uokozi vimepata miili zaidi ya watu leo katika eneo la ajali ya ndege ya shirika la Lion Air iliyoanguka baharini ikiwa na watu 189.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737 Max , ambayo ilifanyiwa matengenezo miezi kadhaa iliyopita, ilianguka katika bahari ya Java muda mfupi baada ya kuomba kurejea mjini Jakarta hapo jana Jumatatu. Mkuu wa Kikosi cha Utafutaji na Uokozi cha Taifa nchini Indonesia Mohammed Syaugi amesema Watafutaji wa miili wamejaza mifuko ya viungo vya binadamu na mabaki[…]

Ndugu jamaa na marafiki MWANZA leo wameungana kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Redio cha idhaa ya Kiswahili Deustchewele (DW) cha nchini Ujerumani marehemu Isaac Muyenjwa Gamba, anayetarajiwa kuzikwa kesho huko wilayani Bunda mkoani Mara

Ndugu, jamaa na marafiki, leo wameungana kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Redio cha idhaa ya Kiswahili Deustchewele (DW) cha nchini Ujerumani marehemu Isaac Muyenjwa Gamba, anayetarajiwa kuzikwa kesho huko wilayani Bunda mkoani Mara. Akiongozi safari ya kuuaga mwili wa marehemu Isaac Muyenjwa Gamba, mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela, amewahasa waandishi[…]