Rais wa Marekani Donald Trump amefuta mkutano wa mazungumzo kati yake na Rais wa Urusi Vladmir Putin aliopanga kuufanya kando na mkutano wa viongozi wa mataifa tajiri zaidi duniani G20.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Trump amesema sababu ya kufuta mkutano huo ni hatua ya Urusi kuendelea kuzishikilia meli za kivita za Ukraine zilizokuwa zikifanya doria kwenye eneo la Crimea hatua inayoongeza mvutano wa kiusalama baina ya mataifa hayo. Aidha Viongozi wa mataifa 20 tajiri zaidi duniani wameendelea kuwasili jijini Buenos Aires nchini Argentina, ikiwa[…]

Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliotarajiwa kufanyika jijini Arusha Tanzania umeahirishwa kutokana na mmoja wa wanachama wa jumuiya hiyo nchi ya Burundi kutohudhuria.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Jamhuri ya Uganda Yowezi kaguta Museveni amesema kwa mujibu wa kanuni za mkataba wa jumuiya hiyo, maamuzi yote ya jumuiya yanatakiwa yafanywe na viongozi wote wa nchi wanachama. Kutokana na hali hiyo Mkutano huo ambao pia Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta alikuwa tayari jijini Arusha[…]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza Kamati za Ulinzi na Usalama kwenye maeneo ya mipakani kuendesha doria za mara kwa mara ili kuwabaini na kuwachukulia hatua watu wote wanaoingia nchini kinyemela bila ya kufuata taratibu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo alipozungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Stendi ya Ushirombo wilayani Bukombe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Geita. Waziri Mkuu alisema ni muhimu kwa viongozi wa maeneo ya kuwa makini katika kufanya ukaguzi kwenye maeneo hayo ili wazuie uingiaji wa wageni kiholela kwa sababu[…]

Waziri Jaffo amemtaka mkuu wa mkoa wa Tabora kuunda tume ya wakaguzi ili kukagua mapato katika mradi wa milango ya maduka inayomilikiwa na halmashauri ya manispaa ya Tabora

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa SELEMANI JAFO amemtaka mkuu wa mkoa wa Tabora kuunda tume ya wakaguzi ili kukagua mapato katika mradi wa milango ya maduka inayomilikiwa na halmashauri ya manispaa ya Tabora kutokana na kusuasua kwa ukusanyaji wa mapato katika mradi huo. Mapema waziri Jafo amewasili[…]

Uingereza inatarajiwa kuikalia kooni Saudi Arabia,kuhusiana na mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi

Uingereza inatarajiwa kuikalia kooni Saudi Arabia,kuhusiana na mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi na Operesheni yake ya kijeshi nchini Yemen. Waziri Mkuu wa Uingereza,Theresa May,amewaambia waandishi wa habari akiwa njiani kuelekea Buenos Aires,Argentina,kwenye mkutano wa nchi 20 zenye viwanda na zinazoinukia,kuwa amenuia kuzungumza na mrithi wa mfalme wa Saudia Mohammed bin Salman,kuhusiana na masuala[…]

Vijana nchini Tanzania wamehaswa kuchangamkia fulsa ya mafunzo ya ujasiliamali kupitia elimu ya masoko ili kujiongezea kipato

Vijana nchini Tanzania wamehaswa kuchangamkia fulsa huru kupitia elimu ya masoko ili kujiongezea kipato na hatimaye kujikwamua katika umasikini . Hayo yamesema na kijana mdogo kutoka nchi ya Afrika ya kusini Sandle Shenzi ambaye amekuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuwapa vijana elimu ya Biashara huru ambayo itafanyika kesho katika ukumbi wa Mwalimu Juliasi Nyerere[…]

Wakazi vingunguti kuelekea machinjioni hadi eneo la barakuda wamelalamikia ubovu wa barabara katika eneo hilo na kusababisha uharibifu wa vyombo vya moto

Wakazi pamoja na waendesha Vyombo vya Moto wanaotumia barabara ya vingunguti kuelekea machinjioni hadi eneo la barakuda wamelalamikia ubovu wa barabara katika eneo hilo na kusababisha uharibifu wa vyombo vya moto lakini pia Msongamano mkubwa wa magari wakati wote. Wakizungumza na chanelten wakazi hao wamesema hali katika barabara hiyo imekuwa mbaya kutokana na mashimo makubwa[…]

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imewaagiza waajiri wote wa utumishi wa umma kuhakikisha wanawapeleka mafunzo ya awali kwa wanasheria wapya wanaowaajiri

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imewaagiza waajiri wote wa utumishi wa umma, kuhakikisha wanawapeleka mafunzo ya awali, wanasheria wapya wanaowaajiri, baada ya rasimu ya mtaala maalum wa sasa kukamilika. Agizo hilo limetolewa jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, BW. MICK KILIBA,[…]

Mfululizo wa video zinazotengenezwa kwa kufuata nukuu anazopenda rais wa China watangazwa duniani

Kabla ya Rais Xi Jinping wa China kuhudhuria Mkutano wa kilele wa G20 na kufanya ziara nchini Argentina, mfululizo wa video za lugha ya Kihispania zilizotengenezwa kwa kufuata nukuu anazopenda rais Xi, zimetangazwa katika nchi zinazozungumza lugha ya kihispania kote duniani kuanzia tarehe 29. Sherehe ya uzinduzi pia ilifanyika siku hiyo mjini Buenos Aires, Argentina.[…]

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kukamatwa kwa Mkaguzi wa ndani katika halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Gavana Mwaitesa, pamoja na Abdallah Nyoni aliyekuwa mhasibu wa Wilaya ya Mbogwe ambapo wote wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kukamatwa kwa Mkaguzi wa ndani katika halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Gavana Mwaitesa, pamoja na Abdallah Nyoni aliyekuwa mhasibu wa Wilaya ya Mbogwe kabla ya kuhamishiwa kwenye Wilaya hiyo, ambapo wote wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo. Waziri Mkuu ambaye amehitimisha ziara yake ya kukagua shughuli za[…]