Hatimaye kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike amemuita kiungo Shiza Ramadhani Kichuya katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mchezo dhidi ya Lesotho

Hatimaye kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike amemuita kiungo Shiza Ramadhani Kichuya katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mchezo dhidi ya Lesotho katikati ya mwezi huu kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Cameroon. Taifa Stars watakuwa wageni wa Mamba wa Lesotho Novemba 18, mwaka huu Uwanja wa[…]

Watu saba wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyotokea barabara kuu ya Dodoma Morogoro eneo mbande wilayani kongwa mkoani Dodoma.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo nakuhusisha magari matatu, ambapo mawili kati yake ni magari ya serikali yenye namba za usajili STL 6250 mali ya ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na lingine ni SU 41173 mali ya mfuko wa hifadhi za jamii wa PSSSF na lori la mizigo aina[…]

Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewataka wahitimu wa mafunzo wa jeshi la akiba Mkoa wa Dsm kujiepusha au kutojiunga na makundi ya wahalifu na badala yake wawe wazalendo katika kuimarisha ulinzi na Usalama katika mitaa yao

Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewataka wahitimu wa mafunzo wa jeshi la akiba Mkoa wa Dsm kujiepusha au kutojiunga na makundi ya wahalifu na badala yake wawe wazalendo katika kuimarisha ulinzi na Usalama katika mitaa yao sambamba na kushiriki kazi za kijamii katika mitaa yao. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa[…]

Wakazi wa kijiji cha Nkungwe wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma wameipongeza serikali kuanza kutatua changamoto ya ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu katika mto Luiche

Wakazi wa kijiji cha Nkungwe wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma wameipongeza serikali kuanza kutatua changamoto ya ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu katika mto Luiche ambapo kuharibuka kwake tangu Agosti mwaka jana kulichangia kuzorota kwa shughuli za kilimo, usafrishaji wa mazao pamoja na chakula, kwani wananchi walilazimika kutumia mitumbwi isiyo salama kutoka upande mmoja[…]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa mfumo wa reli ya kisasa (SGR) inayojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kuanzia eneo la Shaurimoyo Dar es Salaam hadi Soga, Pwani, ambapo ameelezwa na wataalam wa ujenzi kuwa kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 ambacho kilitakiwa kukamilika Julai 2019, watakikamilisha Aprili 2019. Waziri Mkuu amebainisha kwua Serikali[…]

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema amri ya kumuua Jamal Khashoggi ilitoka kwa watu wa ngazi ya juu katika serikali ya Saudi Arabia huku akiapa kutokata tamaa katika msako wa waliomuua.

Akizungumza jana, ikiwa ni mwezi mmoja baada ya Khashoggi kuuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul, Erdogan amesema haamini hata kidogo kuwa Mfalme Salman anapaswa kulaumiwa. Lakini alishindwa kumuondolea lawama Mwanaflame mrithi Mohammed bin Salman kwa kumtumia kikosi cha wauwaji mwanahabari huyo wa Saudia ambaye kifo chake kimeichafua hadhi ya kiongozi huyo. Katika tahariri[…]

Wakristo wa madhehebu ya Koptik wanajiandaa kuwazika waumini wao waliouwawa katika mji wa Minya kusini mwa Mji Mkuu wa Misri Cairo.

Kanisa hilo la Koptik pamoja na Wizara ya mambo ya ndani ya Misri wanasema wanamgambo wa Kiislamu waliyavamia mabasi matatu yaliyokuwa yamewabeba mahujaji wa Kikristo kuwapeleka katika nyumba moja ya utawa iliyoko jangwani. Watu saba waliuwawa na wengine kumi na tisa kujeruhiwa. Kulingana na orodha ya majina iliyotolewa na kanisa hilo watu wote waliouwawa isipokuwa[…]

Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umesababisha vifo vya watu 180.

Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini humo, Kuna vifo kumi ambavyo vimetokea katika siku za hivi karibuni. Wizara ya Afya imesema jana kuwa imesajili matukio 285 yanayoweza kuthibitika kuwa Ebola na vifo 180. Mripuko wa hivi karibuni unasambaa kwa kasi katika eneo linalokumbwa na machafuko la Kaskazini mashariki jimbo la Kivu Kaskazini ambayo ni[…]