CCM kupitia vyombo vyake vya habari kimeanza uhakiki wa wafanyakazi hewa ili kujiridhisha na kubaini kama kuna wafanyakazi ambao wako katika orodha ya malipo ya mishahara ambao ni hewa.

Chama cha Mapinduzi kupitia vyombo vyake vya habari kimeanza uhakiki wa wafanyakazi hewa ili kujiridhisha na kubaini kama kuna wafanyakazi ambao wako katika orodha ya malipo ya mishahara ambao ni hewa. Akizungumza waandishi wa habari jijini Dar es saalam, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa vyombo vya habari vya chama cha mapinduzi Ernest Sungura amesema katika kuhakikisha[…]

Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM limewataka wanachi wote katika jiji la DSM kujiepusha na Vitendo vya uvunjifu wa Amani katika Mkesha wa Kuukaribisha Mwaka mpya,kuchoma matairi barabarani pamoja na kufyatua fataki.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limewataka wanachi wote katika jiji la dsm kujiepusha na Vitendo vya uvunjifu wa Amani katika Mkesha wa Kuukaribisha Mwaka mpya,kuchoma matairi barabarani pamoja na kufyatua fataki bila kibali cha jeshi hilo. Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Kamishna Msaidizi wa Polisi Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa[…]

Januari 2 saa nne asubuhi Dkt. Shein anatarajiwa kuzindua vituo vya Uokozi vya KMKM kwa niaba ya Vituo vya Uokozi vya KMKM vya Kibweni na Nungwi hafla itakayofayika katika Bandari ya Mkoani Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amerejea visiwani Zanzibar jana akitokea nchini Uingereza na kulakiwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Idd. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Zanzibar, Dkt. Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mazoezi[…]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Matambalale wilayani Ruangwa ukamilike kwa wakati na kwa viwango vilivyosudiwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Matambalale wilayani Ruangwa ukamilike kwa wakati na viwango vilivyosudiwa huku akiwataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana na kuhakikisha wanachangia nguvukazi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ili mwakani wanafunzi waanze kusoma. Waziri Mkuu alikuwa akizungumza wilayani Ruangwa mkoani Lindi alipotembelea eneo la[…]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema jumla ya shilingi bilioni 222 zimelipwa na Serikali kwa wakulima wa zao la korosho na kutaka wakulima wawe na subira.

Amesema wakulima walioanza kulipwa ni wale wenye kilo zisizozidi kilo 1,500 na wale wenye kilo zaidi ya 1,500 na kuendelea Serikali inaendelea na uhakiki kisha watalipwa huku akisisitiza kuwa hakuna mkulima ambaye atapoteza haki yake. Waziri Mkuu ameyasema hayo jana Desemba 30 akiwa katika ziara wilayani Ruangwa mkoani Lindi alipozungumza na wananchi wa kijiji cha[…]

Rais Xi Jinping wa China atoa hotuba ya kukaribisha mwaka mpya wa 2019

Rais Xi Jinping wa China leo tarehe 31 Desemba ametoa salamu za mwaka mpya kupitia Kituo kikuu cha radio na televisheni cha taifa cha China na mtandao wa Internet, ambapo amewatakia wachina wote heri ya mwaka mpya wa 2019. Tusikilize hotuba yake. Makomredi, marafiki, mabibi na mabwana, Hamjambo! “Wakati hausimami, na msimu hutiririka kama maji”.[…]

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana Desemba 30

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana Desemba 30 baada ya kuahirishwa mara kadhaa nchini humo. Hata hivyo wagombea wakuu wa upinzani Felix Tshisekedi na Martin Fayulu wamelalamikia walichodai dosari nyingi zilitokea wakati wa uchaguzi huo. Felix Tshisekedi, mtoto wa mkongwe wa upinzani nchini DRC,[…]

Rais wa Marekani Donald Trump amesema amefanya mazungumzo marefu na Rais wa China Xi Jinping na kudai kuwa mpango wa kuyarejesha mahusiano ya biashara baina ya nchi hizo mbili unaendelea vyema.

Rais Trump ametoa kauli hiyo huku shughuli za serikali kuu katika baadhi ya idara za Marekani zikiwa bado zimekwama kwa siku ya nane leo na kukiwa hakuna dalili yeyote ya kupatikana suluhu hivi karibuni Marekani na China zimekuwa katika vita vya kibiashara kwa sehemu kubwa ya mwaka 2018 jambo lililoyumbisha biashara ya dunia ambapo nchi[…]

Chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma kimesema kitamkumbuka mkongwe wa chama hicho Mzee Pancras Ndejembi kwa juhudi zake za kuufanya mkoa huo kuwa ngome ya CCM.

Chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma kimesema kitamkumbuka mkongwe wa chama hicho Mzee Pancras Ndejembi kwa juhudi zake za kuufanya mkoa huo kuwa ngome ya CCM na kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Dodoma inabaki kwenye kumbukumbu ya baba wa taifa mwalimu nyerere ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi. Hayo yameelezwa na[…]

Baadhi ya wakulima wa zao la pamba katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Urambo mkoani Tabora wamejikuta katika hali ya sintofahamu baada ya kiasi cha pamba iliyozalishwa msimu uliopita kushindwa kununuliwa.

Baadhi ya wakulima wa zao la pamba katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Urambo mkoani Tabora wamejikuta katika hali ya sintofahamu baada ya kiasi cha pamba iliyozalishwa msimu uliopita kushindwa kununuliwa kutokana na pamba hiyo kuwa fifi, hivyo wameiomba serikali iwasaidie ili pamba hiyo daraja B iweze kununuliwa hatua ambayo itawajengea matumaini mapya katika msimu[…]