TRA mkoani Njombe imeyakamata malori sita yaliyokuwa yakisafirisha bidhaa za mbao na mkaa kwa tuhuma za kutokuwa na risiti za EFD.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Njombe imeyakamata malori sita yaliyokuwa yakisafirisha bidhaa za mbao na mkaa kwa tuhuma za kutokuwa na risiti za EFD kitendo ambacho kinadaiwa kuwa na lengo la kukwepa kulipa kodi. Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Njombe, Musibu Shabani akizungumza katika eneo la tukio la ukaguzi wa magari[…]

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema madai ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa Bunge halijamlipa fedha zozote tangu ashambuliwe hayana ukweli.

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema madai ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa Bunge halijamlipa fedha zozote tangu ashambuliwe hayana ukweli kwani hadi kufikia Mwezi Desemba mwaka jana Bunge limemlipa malipo mbalimbali yapatayo shilingi milioni 250. Spika amefikia uamuzi wa kulieleza Bunge kuhusu fedha ambazo amelipwa Mbunge huyo Tangu ashambuliwe Tarehe 07 Septemba[…]

Idadi ya waliopotea maisha baada ya boti waliyokuwa wakisafiria zaidi ya watu 130 kuzama nje ya Pwani ya Djibout imeongezeka na kufikia 52.

Mkuu wa Ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji nchini Djbouti IOM Lalini Veerassamy amesema Boti mbili zilizobeba Raia wa Ethiopia zilizama muda mfupi baada ya kuondoka Djibout kutokana na mawimbi makubwa ya bahari yaliyokuwa yakivuma Kikosi cha ulinzi katika Pwani ya Djibouti kinaendelea kutafuta watu waliotoweka kwa matumaini ya kuwapata wakiwa bado hai. Wahamiaji[…]

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela ambaye amejitangaza kuwa Rais wa mpito, Juan Guaido amedai kuwa amefanya mikutano ya siri na jeshi pamoja na vikosi vya usalama vya nchi hiyo akitafuta kuungwa mkono.

Kauli hiyo imo katika maoni yake yaliyochapishwa katika Gazeti la New York Times toleo la leo ambapo amesema kipindi cha mpito kinahitaji kuungwa mkono na Jeshi la nchi hiyo ili kufanukisha mabadiliko. Jana yalifanyika maandamano mengine mapya kumshinikiza Rais Nicolas Maduro ambaye alishinda uchaguzi wa Urais hivi karibuni aachie madaraka pamoja na kulishinikiza jeshi kuruhusu[…]

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imeipiga kalenda kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe na wenzake.

Kesi hiyo iliyokuwa inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye ameteuliwa kuwa Jaji, imetajwa leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kevin Mhina. Wakili wa Serikali, Wankyo Simon ameieleza mahakama kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanarufaa maalum ambayo bado haijasikilizwa, hivyo wameiomba mahakama kuahirisha, maombi ambayo hakimu Mfawidhi Mhina amekubaliana nayo[…]

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa AFADHALI TWALIBU AFADHALI amewataka watendaji wa serikali kushirikiana na viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika kutekeleza ilani ya CCM ambayo inalenga zaidi kuwaletea wananchi maendeleo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa AFADHALI TWALIBU AFADHALI amewataka watendaji wa serikali kushirikiana na viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika kutekeleza ilani ya CCM ambayo inalenga zaidi kuwaletea wananchi maendeleo badala ya kuendekeza migogoro isiyokuwa na tija. Ametoa wito huo akiwa mjini Tabora katika kuhitimisha ziara yake ambapo alitembelea wilaya zote za mkoa[…]

Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za ujangili na uuaji wa wanyapori wakiwemo Twiga wilayani Longido ambapo katika kipindi cha mwaka 2017 /2018 ambapo Twiga 25 waliuawa.

Hayo yamebainishwa jijini Arusha wakati wa kamati maalumu ya kufuatilia ujangili wa Wanyamapori wilayani Longido hususani Twiga ikiwasilisha taarifa kwa mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo, ambapo imebainika katika kipindi cha miaka miwili Jumla ya twiga 35 wameuwawa kwa sababu mbalimbali ambapo kati yao twiga 25 walioouawa kwa ujangili Jumla ya twiga 24 walioripotiwa kuuawa ndani[…]

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka arobaini na miwili ya Chama cha Mapinduzi CCM ambayo kwa mkoa wa Pwani yanatarajiwa kufanyika wilayani Mkuranga.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani RAMADHANI MANENO , pamoja na shughuli nyingine pia Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ataweka jiwe la msingi katika jengo la kitega uchumi la CCM wilaya ya Mkuranga. Aidha mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Pwani RAMADHANI MANENO .akaainisha shughuli zitakazofanywa katika maadhimisho[…]

Siku moja baada ya Utawala wa Kisoshalisti nchini Venezuela kumpiga marufuku Kiongozi wa Upinzani Juan Guaido kuondoka nchini humo, kiongozi huyo ameendelea kuhamasiha migomo.

Siku moja baada ya Utawala wa Kisoshalisti nchini Venezuela kumpiga marufuku Kiongozi wa Upinzani Juan Guaido kuondoka nchini humo wakati akichunguzwa kuhusina na vitendo vyake dhidi ya Serikali ya Rais Nocolas Maduro, Kiongozi huyo anaendelea kuhamasiha migomo nchini humo. Ongezeko la mvutano wa kisiasa limebabisha mataifa zaidi ya 12 ikiwemo Marekani pamoja na mataifa mengine[…]

Baadhi ya wateja wakubwa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakiwemo wamiliki wa viwanda katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, wamezungumzia kuimarika kwa hali ya umeme katika mikoa hiyo.

Baadhi ya wateja wakubwa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakiwemo wamiliki wa viwanda na wale wanaotoa huduma muhimu zinazohitaji umeme mwingi, kama viwanja vya ndege, katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, wamezungumzia kuimarika kwa hali ya umeme katika mikoa hiyo,jambo ambalo limerahisisha zaidi shughuli zao tofauti na ilivyokuwa awali. Timu ya wahariri waandamizi kutoka[…]