Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara kupeleka muswada Bungeni kwa ajili ya kuunganisha Taasisi mbili za Serikali ambazo ni TBS na TFDA kutokana na Taasisi hizo kufanana katika utendaji kazi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara kupeleka muswada Bungeni kwa ajili ya kuunganisha Taasisi mbili za Serikali ambazo ni Shirika la Viwango Tanzania TBS pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kutokana na Taasisi hizo kufanana katika utendaji kazi pamoja na kupunguza urasimu uliolalamikiwa kwa muda mrefu na Wafanyabishara nchini[…]

Wachimbaji wadogo wa dhahabu wawili katika mgodi wa Bulumbaka, uliopo Kata ya Gasuma, Wilayani Bariadi mkoani Simiyu, wamefariki Dunia, baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakiwa ndani ya mashimo wakichimba dhahabu, huku Serikali ikifunga baadhi ya mashimo ya mgodi huo.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga ambaye alikesha katika eneo hilo mara baada ya kupata taarifa za kutokea kwa tukio hilo jana majira ya saa tisa alasiri, anasema wamefanikiwa kutoa miili ya watu wawili ambao walifukiwa na kifusi wakiwa ndani ya mashimo hayo wakichimba dhahabu. Kwa upande wake Afisa Madini wa Mkoa wa Simiyu,[…]

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Februari 28 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) . Kazuhiko Koshikawa.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto. Rais Magufuli ameishukuru JICA kwa kuwa mdau muhimu wa maendeleo ya Tanzania na amemhakikishia Bw. Koshikawa kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi[…]

Moto mkubwa umezuka katika Maghala yaliyo ndani ya kiwanda cha bora kilichopo maeneo ya Tazara jijini Dar es Salaam na kuteketeza shehena za bidhaa zilizokuwa zimehifadhiwa katika maghala hayo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana umetokea majira ya saa kumi na moja alfajiri katika ghala moja ya kuhifadhia bidhaa mali ya kampuni ya somi chem na baadae kusambaa katika ghala za bidhaa za kampuni ya DIY LTD pamoja ghala la kampuni ya bia ya Serengeti. Kwa[…]

Rais wa Marekani Donald Trump amesema mkutano wa kilele kati yake na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mjini Hanoi, Vietnam umekamilika bila ya kufikiwa makubaliano kwa sababu hakuwa tayari kuiondolea Korea Kaskazini vikwazo.

Rais Trump amewaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini ilitaka vikwazo vyote ilivyowekewa kuondolewa jambo ambalo Marekani haingeweza kulitekeleza. Hata hivyo Rais Trump amesisitiza kuwa bado wana uhusiano mzuri na Kiongozi wa Korea Kaskazini licha kupishana katika vipengele kadhaa katika mazungumzo yao. Awali, viongozi hao walikuwa wameonyesha matumaini ya kuimarisha mahusiano na kupiga hatua katika[…]

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka wafanyakazi na wananchi wanaozunguka Mradi wa Reli ya Kisasa SGR kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu badala yake watoe ushirikiano kwa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga mradi huo unaotumia fedha za ndani za Watanzania.

Akizungumza wakati alipofanya ziara kwenye mradi huo kutoka kituo cha Ilala hadi Kilosa mkoani Morogoro, IGP Sirro amesema kuwa, kila mmoja anayo nafasi ya kufanya ili kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa haraka na katika muda uliopangwa bila kuwa na vikwazo. Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha usalama unakuwepo wakati wote hata[…]

Abiria waliokuwa wanasafiri na basi la kampuni ya Navil Express kutoka Nachingwea mkoani Lindi kuelekea Dar es Salaam wamenusurika baada ya basi lao kugonga ng’ombe mmoja kati ya kundi la ng’ombe lililokuwa linakatisha barabara katika kijiji cha Namakongwa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Wakizungumza katika eneo ilipotokea ajali hiyo,abiria wa basi hilo lenye namba za usajili T420 DDT wamesema kuwa ajali imetokea baada ya kundi la ng’ombe kuingia barabari ghafla ambapo dereva akagonga ng’ombe mmoja wakati anajaribu kuwakwepa ng’ombe hao. Aidha baadhi ya mashuhuda ambao sio abiria wa basi hilo wamesema kuwa ng’ombe hao walikuwa wameibiwa na kwamba[…]

Nchi Nane zinazotekeleza mkataba wa kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi ( ZAMCOM) zimekutana jijini dar es salaam kwa lengo la kujadili mpango mkakati wa miaka 20 uliowekwa ili kulifanya bonde hilo kuwa endelevu na lenye manufaa kwa nchi husika.

Nchi hizo ni Angola, Botswana, Msumbiji, Malawi, Namibia, Zambia, Zimbabwe, na Tanzania ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo ambapo zitajadili mikakati ya kuendeleza mto zambezi na ziwa nyasa kwa maslahi mapana ya nchi hizo. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliowakutanisha mawaziri wanane kutoka nchi hizo Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa ambaye anakabidhi[…]

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara, na taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu kuhakikisha zinapeleka vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinavyozingatia teknolojia mpya.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara, na taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu kuhakikisha zinapeleka vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinavyozingatia teknolojia mpya kulingana na mitaala ya serikali pamoja na kusambaza walimu katika vituo vya wenye uhitaji maalumu nchini ili kusaidia jamii hiyo kupata elimu bora inayokwenda na sambamba na soko la ajira.[…]

Mgombea urais wa chama tawala nchini Nigeria aliyekuwa akitetea kiti hicho Rais Muhammadu Buhari ameibuka mshindi wa uchaguzi uliofanyika Jumamosi Februari 23.

Kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi (INEC), Buhari amepata asilimia 56 ya kura zote zilizopigwa hivyo kumpa uhalali wa kuiongoza nchi hiyo ya Afrika magharibi kwa miaka mingine minne. Hata hivyo awali upinzani ulilalamikia kuwepo kwa njama za kuiba kura na kudai kwamba hautokubali matokeo hayo Habari zinasema Buhari ameshinda kwa[…]