Shirika la Reli Tanzania limesema kuwa milango bado ipo wazi kwa makundi mbalimbali kuutembelea mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR inayojengwa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa lengo la kujifunza kama walivyofanya wasanii mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kungu Kadogosa mara baada ya kupokea wasanii,wanamichezo na washereheshaji zaidi ya 300 waliotembela mradi wam Ujenzi wa Reli hiyo ya kisasa. Wasanii hao walitumia usafiri wa treni ya delux na kushuhudia ujenzi wa Reli hiyo wakiwa ndani ya treni hiyo ambapo pia walikuwa wakishuka na kujionea[…]

Serikali kupitia kitengo cha urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya Rushwa imefanikiwa kuokoa zaidi shilingi Bilioni 127, kutaifisha akaunti zenye thamani ya bilioni 4.5 pamoja na kushinda kesi 685 kati ya 1340.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dk. Marry Mwanjelwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum Fakharia Khamis aliyehoji Mkakati wa serikali kulinusuru taifa dhidi ya rushwa. Akijibu swali hilo Dk. Mwanjelwa amesema kupitia kitengo hicho cha kurejesha, kutaifisha na kuokoa mali zilizopatikana kwa njia ya rushwa chini[…]

Jeshi la Polisi la Dorset limethibitisha kwamba Mwili ulioopolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege iliyoanguka ni wa mchezaji soka wa timu ya Cardiff City, Emiliano Sala.

Sala, aliyekuwa na umri wa miaka 28, alikuwa akisafiri kwenda Cardiff katika ndege ambayo,rubani wake alikuwa ni David Ibbotson, ilipotea mnamo Januri 12. Kwa mujibu wa BBC. Mwili wake ulipatikana Jumatano baada ya kugunduliwa kwa mabaki ya ndege hiyo Jumapili asubuhi. Polisi ya Dorset imethibitisha utambulisho wake Alhamisi usiku katika taarifa yake, kikosi hicho kimesema[…]

Umoja wa mataifa pamoja na Shirika la Kimataifa la Hilali Nyekundu nchini Syria SARC wamepeleka msafara wa magari yaliyosheheni misaada ya kibinadamu kwa ajili takriban zaidi ya watu 40000 walipoteza makazi na wanaohitaji msaada wa haraka waliopo katika kambi iliyopo kusini mwa Syria.

Umoja wa mataifa pamoja na Shirika la Kimataifa la Hilali Nyekundu nchini Syria SARC wamepeleka msafara wa magari yaliyosheheni misaada ya kibinadamu kwa ajili takriban zaidi ya watu 40000 walipoteza makazi na wanaohitaji msaada wa haraka waliopo katika kambi iliyopo kusini mwa Syria. Msafara huo tayari umeshawasili katika mji wa Rukban na unatajwa kuwa msaada[…]

Malori yaliyobeba msaada wa kiutu unaohitajika kwa dharura nchini Venezuela yameanza kuwasili katika mpaka wa nchi hiyo na Colombia.

Malori kadhaa yaliyobeba chakula na dawa yaliingia katika kituo cha ukusanyaji katika upande wa Colombia wa daraja la Tienditas, ambalo mpaka sasa limefungwa na wanajeshi wa Venezuela na hivyo kufanya zoezi la kugawa misaada kuwa gumu. Msafara huo ulioondoka siku moja kabla kutoka kaskazini mashariki mwa Colombia, ulishangiliwa na wahamiaji wa Venezuela baada ya kuwasili[…]

Sakata la mauaji ya twiga zaidi ya 25 kutokana na ujangili wilayani Longido limeendelea kuchukua sura mpya baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuunda kamati nyingine maalumu.

Sakata la mauaji ya twiga zaidi ya 25 kutokana na ujangili wilayani Longido limeendelea kuchukua sura mpya baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuunda kamati nyingine maalumu chini ya mkuu wa Wilaya ya Longido James Mwaisumbe ambayo italazimika kuwahoji watuhumiwa wote watano wanaohusishwa na jambo hilo kabla ya kupelekwa mahakamani, pamoja na[…]

Ili kukabiliana na kutokomeza ukeketaji hapa nchini serikali imeombwa kuingiza somo la ukeketaji katika mitaala ya elimu ya sekondari na msingi kuepuka kuendelea kupoteza wanawake.

Ili kukabiliana na kutokomeza ukeketaji hapa nchini serikali imeombwa kuingiza somo la ukeketaji katika mitaala ya elimu ya sekondari na msingi kuepuka kuendelea kupoteza wanawake ambao wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kuvuja damu nyingi kipindi cha kujifungua ambapo mkoa wa Manyara unatajwa kuongoza kwa ukatili huo kwa 58% kwa mujibu takwimu za 2015-2016. Hilo ni[…]

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wamelalamikia kitendo cha baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya ya Wilaya ya Bariadi Vijijini na maofisa wa madini kuwatoza ushuru bila kuwapa risti.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Mashamba ya Kijiji cha Bulumbaka Kata ya Mwaobingi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Vijijini, mkoani Simiyu na wajasiliamali wadogo katika machimbo hayo, wamelalamikia kitendo cha baadhi ya watendaji wa Halmashauri hiyo na maofisa wa madini kuwatoza ushuru bila kuwapa risti. Wakizungumza kwa hisia kali, wachimbaji hao wa dogo[…]