Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Humphrey Polepole ameiagiza kampuni ya CHINA WU inayojenga barabara ya kilometa 49.5 kutoka Waso-Sale kuzingatia suala la usalama mahala pa kazi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Humphrey Polepole ameiagiza kampuni ya CHINA WU inayojenga barabara ya kilometa 49.5 kutoka Waso-Sale kuzingatia suala la usalama mahala pa kazi kwa kuboresha mazingira ya kuishi wafanyakazi,mishahara na vitendea kazi tofauti na ilivyosasa ambapo wafanyakazi hao wanaishi na kufanyakazi katika mazingira magumu na hatarishi. Bwana Polepole[…]

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesisitiza suala zima la maadili kwa viongozi ikiwa ni pamoja na kujua wajibu wao na wanaowaongoza.

Rais Dk. Shein ameyasema hayo leo mjini Zanzibar katika Majumuisho ya ziara yake ya Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo viongozi mbalimbali wamehudhuria. Katika hotuba yake Dkt. Shein amesema kuwa kiongozi anapaswa kuwa na maadili mazuri ili iwe rahisi katika utendaji wake wa kazi hatua ambayo itawasaidia mpaka wale anaowaongoza kutekeleza wajibu wao[…]

Wakazi wanaotumia barabara ya Shekilango na Morogoro jiji Dar es salaam leo wamejikuta katika wakati mgumu kwa muda wa saa moja kufuatia Lori kubwa aina ya Semi Trailer kuharibika kwenye makutano ya barabara hizo hivyo kusababisha msongamano wa magari .

Wakazi wanaotumia barabara ya Shekilango na Morogoro jiji Dar es salaam leo wamejikuta katika wakati mgumu kwa muda wa saa moja kufuatia Lori kubwa aina ya Semi Trailer kuharibika kwenye makutano ya barabara hizo hivyo kusababisha msongamano wa magari . Camera ya Channel Ten imenasa tukio hilo na kujionea hali ilivyokuwa kufuatia magari mwendokasi kushindwa[…]

Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya radio duniani leo baadhi ya wananchi wameelezea umuhimu wa chombo hicho katika kufikisha ujumbe na taarifa mbalimbali muhimu kwa umma kwa haraka.

Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya radio duniani leo baadhi ya wananchi wameelezea umuhimu wa chombo hicho katika kufikisha ujumbe na taarifa mbalimbali muhimu kwa umma kwa haraka na hivyo kuchochea maendeleo ya kijami na kiuchumi. Channel Ten imezungumza na baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam ambao wamesema, kutokana na kukua kwa[…]

Waziri Dkt. Medard Kalemani ametoa mwezi moja kwa mkandarasi anayejenga mradi wa kuboresha huduma za umeme kuelekea wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ametoa mwezi moja kwa mkandarasi anayejenga mradi wa kuboresha huduma za umeme kuelekea wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam kamilisha na kuwasha rasmi mradi huo ili kuondoa kero ya kukosekana kwa nishati ya umeme kwa wananchi wa wilaya hiyo. Akizungumza wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya mradi huo Dkt[…]

Mbunge wa Iramba Magharibi Dkt. MWIGULU NCHEMBA pamoja dereva wake wamenusurika katika ajali iliyotokea baada gari alilokuwa akisafiria kugonga punda katika maeneo ya Migori Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, mara baada ya kumpokea mbunge huyo na kupatiwa huduma, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dk. Alphonce Chandika amefafanua kuwa Dk. NCHEMBA alikuwa akilalamika kuwa na maumivu katika maeneo ya kifua na kiuno. Naye, Mbunge huyo wa Iramba Magharibi amemshukuru Mungu kuwanusuru yeye na dereva wake katika[…]