Wakazi zaidi ya elfu mbili wa vitongoji vya Migombani na Mbuyuni vilivyopo kijiji cha Kilambo wilayani Mtwara wamelazimika kuyahama makazi yao kwa kutumia mitumbwi huku ekari zaidi ya 925 za mpunga na ekari zaidi ya 500 za mahindi zikiharibiwa na mafuriko.

Wakazi zaidi ya elfu mbili wa vitongoji vya Migombani na Mbuyuni vilivyopo kijiji cha Kilambo wilayani Mtwara wamelazimika kuyahama makazi yao kwa kutumia mitumbwi huku ekari zaidi ya 925 za mpunga na ekari zaidi ya 500 za mahindi zikiharibiwa na mafuriko ya mto Ruvuma yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali. Wakiwa kwenye[…]

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Lucas Luhende Kija kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Taifa kwa Watu Wenye Ulemavu. Dkt. Kija ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE).

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Michael Pius Nyagoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA). Bw. Nyagoga ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Sera, Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa wenyeviti[…]

Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL limepewa siku 30 kuhakikisha maeneo yote ambayo hayana kadi za simu na vocha za simu za mtandao huo zinawafikia.

Akizungumza alipotembelea makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye amesema haifai kuona maeneo ya vijijini bado hayapati huduma za mawasiliano kwa ufanisi. Naibu Waziri Nditiye ametoa mwezi moja kwa shirika hilo kutatua changamoto ya upatikanaji wa kadi za simu pamoja na vocha za simu[…]

Mradi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia maporokomo ya maji ya mto rufiji , maarufu kama Stigliers Gorge umekabidhiwa rasmi kwa wakandarasi Arab contractors na Osman A Osman za kutoka nchini Egypt.

Hafla ya kukabidhi eneo la mradi imesimamiwa na waziri wa nishati Medard Kalemani ambapo utekelezaji wa mradi uantarajiwa kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla katika kufikia azma ya serikali ya Tanznia ya viwanda pamoja na kupunguza gharama za umeme uatakapokamilika. Waziri wa nishati Dr Medard Kalemani, amewataka wakandarasi watakaohusika na ujenzi wa mradi[…]

Norway pamoja na Iran zimepongeza rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya ikiwemo za utekelezaji wa miradi mikubwa ya Maendeleo, uboreshaji wa huduma za kijamii, Utawala bora na Uwajibikaji pamoja na maapambano dhidi ya rushwa huku zikiahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania.

Norway pamoja na Iran zimepongeza rais Dkt, John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya ikiwemo za utekelezaji wa miradi mikubwa ya Maendeleo, uboreshaji wa huduma za kijamii, Utawala bora na Uwajibikaji pamoja na maapambano dhidi ya rushwa huku zikiahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uwekezaji na utalii. Kauli hizo zimetolewa[…]

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole amesema serikali ya CCM inayoongozwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeamua kujikita katika siasa ya maendeleo na si za madaraka.

Bwana Polepole ambae anaendelea na ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika wilaya na kata zote za mkoa wa Arusha yupo wilayani Arumeru akianzia halmashauri ya Arusha anatembelea hospitali ya wilaya ya ORTUMET ,shule ya Mwandeti na IRKIDING’A huku akushiriki katika ujenzi wa majengo hayo[…]

Kamishna Jenerali wa idara ya uhamiaji nchini (CGI) Anna Makakala ametembelea mkoani Pwani kwa ajili ya kuangalia vipenyo wanavyopitia wahamiaji haramu.

Kamishna Jenerali wa idara ya uhamiaji nchini (CGI) Anna Makakala ametembelea mkoani Pwani kwa ajili ya kuangalia vipenyo wanavyopitia wahamiaji haramu pamoja na bandari bubu ikiwani mkakati wa kudhibiti biashara hiyo haramu. Ziara ya Kamishina Jenerali wa idara ya Uhamiaji nchini ambaye ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Pwani ilianza katika[…]

Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd amewataka wanachama wa chama cha Mapinduzi, CCM, nchini kuvunja makundi na kuunganisha nguvu na umoja wanapokabiliana na ushindani wa kisiasa.

Balozi Seif ally Idd ambaye pia ni mlezi wa chama cha mapinduzi, mkoa wa Shinyanga, ametoa rai hiyo mjini hapa katika kilele cha maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM zoezi lililokwenda sambamba na kupokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani. Amesema hakuna haja ya kuendeleza malumbano ndani ya chama badala yake kusaidia jitihada[…]

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa Shehiya ya Kianga, Wilaya Magharibi ‘A’ kukitunza vyema pamoja na kukitumia ipasavyo kituo cha Afya, ili kiweze kuwa endelevu na kuleta tija kwa jamii.

Dkt. Shein alikuwa ajizungumza katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la msingi la Kituo cha Afya Kianga, kilichojengwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa ushirikiano na wananchi ambapo amesema suala la upatikanaji wa huduma bora za Afya nchini halina mbadala, hivyo kuna haja ya kukitunza kituo hicho na kuhakikisha wananchi wa shehiya hiyo[…]

Mamlaka ya hali ya hewa nchini imetoa tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali nchini ikiwemo menejimenti ya maafa ikiwa, ikiwashauri kuchukua tahadhari kutokana na mvua nyingi zinazotarajiwa kunyesha.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini imetoa tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali nchini ikiwemo menejimenti ya maafa ikiwa, ikiwashauri kuchukua tahadhari kutokana na mvua nyingi zinazotarajiwa kunyesha katika maeneo mengi ya nchi ambazo zinaweza athari nyingine zitokanazo na mvua nyingi kama vile uharibifu wa makazi, miundombinu na hata mafuriko. Kwa mujibu wa mamlaka ya[…]