Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amekilaumu chama kikuu cha upinzani nchini humo kuwa ndio chanzo cha kuahirishwa kwa uchaguzi.

Uchaguzi wa rais uliokuwa ufanyike leo, umesogezwa mbele kwa muda wa wiki moja hadi tarehe 23 mwezi huu wa Februari. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo Mahmood Yakubu ametoa tangazo la kuahirishwa uchaguzi saa chache kabla ya vituo kufunguliwa. Ofisi ya Rais Muhammadu Buhari imedai chama cha Peoples Democratic PDP cha mpinzani wake[…]

Shirika la viwango Tanzania TBS limeteketeza tani 4.5 za bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Milioni 67, baada ya kubainika kuwa na viwango hafifu vya ubora.

Bidhaa zilizotekezwa ni pamoja vifaa vya kuzuia majanga ya hitilafu za umeme na radi majumbani (earth copper), vijiko vinavyotumika kwa matumizi ya nyumbani kama vile kulia chakula, pamoja na makufuli ambavyo vilikamatwa February 2 mwaka huu katika bandari ya Dar es salaa vikiingizwa nchini kutokea China. Afisa Ubora wa Viwango wa TBS Grangay Masala aliyesimamia[…]

Waziri wa katiba na sheria Profesa Palamagamba Kabudi amewataka viongozi wa kitaifa kuweka maslahi ya taifa mbele, kuheshimu mamlaka na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya uongozi kwa kuzingatia mila na desturi za uongozi za jamii ya Kitanzania.

Profesa Kabudi ametoa rai hiyo wakati wa kufunga kozi fupi ya sita ya viongozi mbalimbali wa kitaifa na kusema kila jamii ina mila na desturi za uongozi ambazo lazima ziheshimiwe na ni wajibu wa viongozi kujua namna ya kutathimini mambo mbalimbali ili maamuzi yao yawe chanya kwa jamii wanayoiongoza na hatimaye kutatua changamoto zinazolikabili taifa[…]

Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amewatoa hofu wavuvi ambao hawatumii vifaa haramu wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwamba waendelee na shughuli zao za uvuvi ili mradi wafuate sheria.

Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amewatoa hofu wavuvi ambao hawatumii vifaa haramu wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwamba waendelee na shughuli zao za uvuvi ili mradi wafuate sheria, taratibu na kanuni kwani nia ya serikali si kuzuia kazi hiyo bali zifanyike kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Hofu hiyo imekuja baada ya utekelezwaji wa[…]

Naibu waziri wa fedha na mipango Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea mradi wa reli mpya ya standard gauge na kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

Naibu waziri wa fedha na mipango Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea mradi wa reli mpya ya standard gauge na kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo pamoja na matumizi ya pesa za serikali zinavyotumika katika mradi huo ambao upo katika hatua ya kwanza. Akizungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri Kijaji amesema kuwa wizara yake inatembelea miradi[…]