Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema mauaji ya watoto na wanawake yanayotokea mkoani Simiyu, yanaanzia kwenye familia, hivyo ipo haja ya kutoa elimu kwa familia na watu kuacha kuilaumu Serikali na kwamba kutokana na mauaji hayo.

IGP Sirro anatoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, kabla ya kuzungumza na Wananchi wa Mji wa Lamadi ambapo kumekuwa kukitokea matukio ya mauaji ya watoto na wanawake. IGP Siro anawasili mkoani Simiyu, majira ya saa 4, asubuhi na kufanya kikao cha ndani na Maofisa wa Jeshi la polisi mkoani hapa,[…]

Wananchi zaidi ya 300 wa kijiji cha Kwahemu kata ya Haneti wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma, wamelazimika kuzuia msafara wa Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Prof. Idris Kikula ili kupata muafaka wa kugaiwa vitalu vya kuchimba madini aina ya Gemastone.

Wakizungumza mbele ya Mwenyekiti huyo, wananchi hao wamedai kuwa licha ya kijiji hicho kuwa wazalishaji wakuu wa madini hayo jamii yao imekuwa hainufaiki na uchimbaji huo kutokana na wachimbaji kutochangia shughuli za kijamii kwa mujibu wa sheria za madini. Kijiji hiki kinatajwa kuwa na wananchi zaidi ya 3800, kwa mujibu wa Afisa madini mkazi wa[…]

Zaidi ya nyumba 40 katika mtaa wa Magogoni Kigamboni jijini Dsm zimebomolewa kwa kinachoelezwa kuwa ni hukumu ya amri ya Mahakama.

Zaidi ya nyumba 40 katika mtaa wa Magogoni Kigamboni jijini Dsm zimebomolewa kwa kinachoelezwa kuwa ni hukumu ya amri ya Mahakama baada ya wananchi hao kudaiwa kujenga katika eneo hilo ambalo linadaiwa kumilikiwa na bwana Mtemi Noriega ambaye alifungua kesi tangu mwaka 1992. Kwa mujibu wa wakazi hao ambao wamejikuta katika hali ya sintofahamu kutokana[…]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaahidi wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma kuwaondolea kero inayowakabili ya upatikanaji wa huduma bora za afya.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaahidi wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma kuwaondolea kero inayowakabili ya upatikanaji wa huduma bora za afya kutokana na kukosekana kwa vituo vya afya vyenye uwezo mkubwa wa kutoa huduma katika kata nyingi za Wilaya hiyo. Kauli hiyo imetolewa wakati akizunguzma na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye[…]

Wananchi wanaodaiwa kuvamia maeneo ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Uwanja wa ndege wa Mwanza, wametakiwa kutoyaendeleza maeneo hayo hadi hapo Serikali itakapotoa maamuzi kuhusu hatma ya mgogoro huo.

Agizo hilo limetolewa Jijini Mwanza na jopo la Mawaziri wanane lililoundwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya kushughulikia migogoro ya ardhi kati ya Wananchi na Taasisi mbalimbali nchini. Baada ya jopo hilo linaloongozwa na Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvu kuwasili, na kisha kuelekea katika eneo la Nyamilolerwa[…]

Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wananchi wanaoishi mabondeni kuhama kwa hiyari yao ili kujinusuru na mafuriko yanayoweza kutokea kufuatia mvua zinazotarajiwa kuanza kunyesha mwisho wa mwezi huu.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wananchi wanaoishi mabondeni kuhama kwa hiyari yao ili kujinusuru na mafuriko yanayoweza kutokea kufuatia mvua zinazotarajiwa kuanza kunyesha mwisho wa mwezi huu,huku serikali ikiendelea kusafisha eneo la daraja la Jangwani ambako kila mvua zinaponyesha husababisha kuparaganyika kwa usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam DART.[…]

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakulima wa alizeti mkoani Singida kutumia mkopo walioupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakulima wa alizeti mkoani Singida kutumia mkopo walioupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuendeleza uzalishaji wa mazao ya kimkakati mkoani humo. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kukabidhi hundi ya mfano yenye thamani[…]

Wananchi wa Nigeria wanaendelea kusubiri kupiga kura baada ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika siku ya Jumamosi Februari 16 kuahirishwa hadi Jumamosi Februari 23, 2019.

Wananchi wa Nigeria wanaendelea kusubiri kupiga kura baada ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika siku ya Jumamosi Februari 16 kuahirishwa hadi Jumamosi Februari 23, 2019 hatua ambayo imewashangaza wengi huku baadhi wakitilia shaka iwapo uchaguzi huo utakuwa huru,wa kuaminika na wa wazi. Tume ya uchaguzi nchini Nigeria ilitangaza kuahirisha uchaguzi mkuu kwa juma moja, hatua iliyochukuliwa[…]

Serikali ya Yemen na wawakilishi wa wanamgambo wa kishia-Houthi wamekubaliana kuhusu awamu ya kwanza ya kuwaondoa wanajeshi kutoka mji wa bandari wa Hodeida.

Serikali ya Yemen na wawakilishi wa wanamgambo wa kishia-Houthi wamekubaliana kuhusu awamu ya kwanza ya kuwaondoa wanajeshi kutoka mji wa bandari wa Hodeida na katika bandari za Salif na Ras Isa ambapo Umoja wa mataifa umesema hayo ni makubaliano muhimu yaliyofikiwa. Bandari ya Hodeida ni muhimu kwa kuwa huko ndiko inakofikia misaada ya jumuia ya[…]

Rais wa Syria Bashar al-Assad ametangaza kwamba vita bado vinaendelea nchini mwake, huku akionya Wakurdi, bila hata hivyo kuwataja, kwamba majeshi ya Marekani ambao wanajiandaa kuondoka Syria, hayatawalindia usalama.

Akizungumza na viongozi wa waliochaguliwa kutoka mikoa yaote ya Syria, Bashar al-Assad amesema nchi yake inaendesha “aina nne za vita”: kijeshi, kiuchumi, kimtandao na vita dhi ya rushwa. Wakati huo huo Bashar al-Assad amewatahadharisha Wakurdi, bila hata hivyo kuwataja, kwamba wasitegemei tena msaada kutoka Marekani, huku akiwasihi kujishusha, na kujisalimisha kwani Marekani haitowalindia tena usalama[…]