Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Tanganyaika Mkoani katavi zimeharibu barabara ya kata ya Mnyagala kilometa moja na kuwasababishaia adha wakazi wa kata hiyo.

Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Tanganyaika Mkoani Katavi zimeharibu barabara ya kata ya Mnyagala kilometa moja na kuwasababishaia adha wakazi wa kata hiyo kutokana na mkandarasi kushindwa kuweka madaraja maeneo kolofi kutokana na ufinyu wa bajeti. Channel ten imezungumza na baadhi ya wakazi wa kata ya mnyagala juu ya changamoto hiyo ya ubovu wa barabra na[…]

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja la mto Sibiti,wilayani Mkalama, Mkoani Singida kutawapunguzia wananchi wa Vijiji vya Nyahaa, wilayani Mkalama na Bukundi,wilayani Simiyu gharama za usafiri na usafirishaji.

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja la mto Sibiti,wilayani Mkalama,Mkoani Singida kutawapunguzia wananchi wa Vijiji vya Nyahaa,wilayani Mkalama na Bukundi,wilayani Simiyu gharama za usafiri na usafirishaji wa kati ya shilingi 10,000 na 15,000/= walizokuwa wakitozwa ili waweze kuvuka katika mto Sibiti. Wakizungumzia changamoto walizokuwa wakipata kabla ya daraja la Mto Sibiti kukamilika na gharama walizokuwa wakitozwa[…]

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold anayeshughulikia Afrika na Mashariki ya Kati Dkt. Willem Jacobs, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Dkt. Willem Jacobs aliyeongozanana na washauri wa Barrick Gold Corporation ambao ni RichHaddock, Duncan Bullivant na Wicus du Preez amesema wamekutana na Rais Magufuli ili kumhakikishia kuwa makubaliano yaliyokuwa tarehe 19 Oktoba, 2017watayatekeleza kikamilifu hasa baada ya kampuni kubwa ya uchimbaji dhahabu ya Rand Gold ya Afrika Kusini kuungana na Barrick[…]

Serikali imeruhusu wafanyabiashara wenye vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kuendelea kufanya hivyo siku chache tangu wizara ya kilimo kueleza nia yake ya kusitisha uagizaji wa sukari kutoka nje kwa wazalishaji wa ndani.

Serikali imeruhusu wafanyabiashara wenye vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kuendelea kufanya hivyo siku chache tangu wizara ya kilimo kueleza nia yake ya kusitisha uagizaji wa sukari kutoka nje kwa wazalishaji wa ndani, baada ya majadiliano kati ya wazalishaji hao na wizara ya kilimo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam[…]

Waziri Kakunda, amewahimiza Watanzania kupanda mazao yanayoondoa umasikini ikiwemo Miparachichi, kwani ukiweza kulima zao hilo unaweza kuvuna katika maisha yako yote.

Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda, amewahimiza Watanzania kupanda mazao yanayoondoa umasikini ikiwemo Miparachichi, kwani ukiweza kulima zao hilo unaweza kuvuna katika maisha yako yote. Waziri Kakunda akiendelea na ziara yake Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro, alipata fursa ya kutembelea Kiwanda cha Africado, kinachozalisha miparachichi , ambapo amewahamasisha watanzania kujijengea utaratibu wa uthubutu kwa kununua[…]

Serikali kupitia Wizara ya Maji, imesema ili kutatua kero ya Maji mkoani Simiyu, iliyodumu tangu enzi za ukoloni, itasambaza Maji katika Wilaya zote za Mkoa huo, kupitia mradi mkubwa wa Ziwa Victoria.

Serikali kupitia Wizara ya Maji, imesema ili kutatua kero ya Maji mkoani Simiyu, iliyodumu tangu enzi za ukoloni, itasambaza Maji katika Wilaya zote za Mkoa huo, kupitia mradi mkubwa wa Ziwa Victoria ambao utekelezaji wake utakuwa wa awamu mbili na kwamba awamu ya kwanza utagharimu Shilingi Bilioni 450. Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Mwandoya,[…]

Waziri Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya mawaziri nane walioteuliwa kutembelea na kutatua migogoro baina ya wananchi na mamlaka za hifadhi nchini ameonya mamlaka hizo kuacha kuwabughudhi wananchi waishio maeneo hayo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya mawaziri nane walioteuliwa kutembelea na kutatua migogoro baina ya wananchi na mamlaka za hifadhi nchini ameonya mamlaka hizo kuacha kuwabughudhi wananchi waishio maeneo hayo. Wajumbe hao wa kamati hiyo wanatua hapa eneo la Kimotoro lililopo wilaya ya Simanjiro[…]

Serikali imeisitishia Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kiasi cha fedha kilichokuwa kimebaki kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Kisasa la Magomeni kutokana na kutoridhishwa na maendeleo ya Mradi huo.

Fedha hizo zitarejeshwa tena kwenye Halmashauri hiyo pale Serikali itakaporidhishwa na utendaji kazi wa Halmashauri hiyo wa kuwatumikia wananchi. Akizungumza katika ziara ya mradi wa Kimkakati wa Ujenzi wa soko la Magomeni jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji amesema Serikali ilikwishatoa Shs Bilioni 3.5 kwa Halmshauri hiyo ikiwa[…]