Wakati raia wa Nigeria wakisubiri kufanyika kwa uchaguzi mwishoni mwa wiki hii baada ya tarehe ya awali kuahirishwa, bado kumekuwa na kizungumkuti kufanyika kwa uchaguzi huo licha ya ya Tume ya Uchaguzi (INEC) kuwahakikishia kuwa Uchaguzi huo utafayika.

Wakati raia wa Nigeria wakisubiri kufanyika kwa uchaguzi mwishoni mwa wiki hii baada ya tarehe ya awali kuahirishwa, bado kumekuwa na kizungumkuti kufanyika kwa uchaguzi huo licha ya ya Tume ya Uchaguzi (INEC) kuwahakikishia kuwa Uchaguzi huo utafayika Jumamosi Februari 23, 2019. Hata hivyo ikiwa zimesalia mbili kabla ya kufanyika uchaguzi huo, tume ya uchaguzi[…]

Chanjo mbalimbali za kuzuia magonjwa ya wanyama zilizokuwa zikiagizwa nje kwa gharama kubwa sasa zitaanza kutengenezwa hapa nchini baada ya serikali kujenga viwanda vya kutengeneza chanjo za wanyama.

Chanjo mbalimbali za kuzuia magonjwa ya wanyama zilizokuwa zikiagizwa nje kwa gharama kubwa sasa zitaanza kutengenezwa hapa nchini baada ya serikali kujenga viwanda vya kutengeneza chanjo za wanyama za aina mbalimbali. Katika ziara yake ya kikazi mkoani Pwani Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ametembelea viwanda hivyo vya kutengeneza chanjo vilivyoko katika halmashauri[…]

Mamia ya wananchi wamejitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Meneja Uhusiano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Glory Mziray aliyefariki ghafla Jumanne ya Februari 19 mwaka huu 2019.

Mwili wa marahemu Glory umeagwa katika kanisa la Kilutheri Tanzania KKKT, Tangi Bovu Jijini Dar es Salaam, huku baadhi ya waombolezaji wakimwelezea marehemu kuwa alikuwa mtu makini na mkarimu kwa kila mtu hususani pale linapokuja suala la kazi . Wamesema watamkumbuka kwa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kutumia taaluma yake ya mawasiliano kutangaza utalii.[…]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein amewataka wanafunzi kutilia mkazo suala la elimu ambayo ndiyo dira ya mafanikio katika maisha yao na familia zao.

Dkt. Shein ameyasema wakati akizungumza na wananchi baada ya kuweka kufungua jengo lenye madarasa manne ya skuli sekondari Michenzani wilaya ya Mkoani ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka wafunzi kusoma kwa bidii ili kuongeza ushindani katika kutafuta elimu. Awali Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri amesema wizara yake inaendelea kuboresha miundombinu[…]

Chuo cha Polisi cha Ufundi kimeanza kutoa mafunzo ya udereva Mkoani Mbeya, kwa watu wote wanaoendesha vyombo vya moto lakini hawakupata mafunzo kwenye vyuo vinavyotambuliwa na serikali.

Chuo cha Polisi cha Ufundi kimeanza kutoa mafunzo ya udereva Mkoani Mbeya, kwa watu wote wanaoendesha vyombo vya moto lakini hawakupata mafunzo kwenye vyuo vinavyotambuliwa na serikali ili kupunguza ajali zinazotokana na uelewa mdogo wa matumizi sahihi ya alama za barabarani kwa Madereva. Mtaribu Kiongozi wa Mafunzo ya Sheria za Usalama barabarani Tanzania kutoka Chuo[…]

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amekitaka chuo cha mafunzo ya kilimo MATI kilichopo mkoani humo kinachomiliki eneo la ardhi la hekta 540 kutoa sehemu ya ardhi ukubwa wa hekta mia moja kwa taasisi ya utafiti wa mifugo TALIRI Naliendele.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amekitaka chuo cha mafunzo ya kilimo MATI kilichopo mkoani humo kinachomiliki eneo la ardhi la hekta 540 kutoa sehemu ya ardhi ukubwa wa hekta mia moja kwa taasisi ya utafiti wa mifugo TALIRI Naliendele inayokabiliwa uhaba wa ardhi kwa ajili ya shughuli za utafiti wa mifugo ambapo inamiliki[…]

Wanataaluma wa fani mbalimbali za kisayansi wametakiwa kukutana na wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi mashuleni, ili kuwafahamisha kuhusu fursa zilizopo katika taaluma husika na jinsi ya kuingia.

Witio huo umetolewa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa shule ya Sekondari Azania jijini Dar es salaam wanaochukua michepuo ya Sayansi, ambao wamesema wanapata shida kuzijua fani nyingine za kisayansi, hivyo kuwafanya kuwa na mazoea ya fani zilezile zinazofahamika sana nchini. Wakizungumza na wanataaluma ya ujenzi kutoka bodi ya usajili ya wabunifu[…]

Marekani imesema itaendelea kushirikiana na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania huku pia ikiipongeza Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hatua mbali mbali ya Utekelezaji wa Miradi Mikubwa ya kimaendeleo.

Marekani imesema itaendelea kushirikiana na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania huku pia ikiipongeza Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hatua mbali mbali ya Utekelezaji wa Miradi Mikubwa ya kimaendeleo lakini pia uimarishaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu, maji hususan katika maendeo ya Vijijini. Balozi wa Marekani[…]