Kura zimeanza kuhesabiwa baada ya uchaguzi wa rais uliofanyika hapo jana nchini Nigeria, huku watu wengi wakiwa wamechelewa kupiga kura kutokana na matatizo ya uhaba wa wahudumu na hitilafu za teknolojia.

Kura zimeanza kuhesabiwa baada ya uchaguzi wa rais uliofanyika hapo jana nchini Nigeria, huku watu wengi wakiwa wamechelewa kupiga kura kutokana na matatizo ya uhaba wa wahudumu na hitilafu za teknolojia ambapo matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa mapema wiki ijayo. Rais ambaye yuko madarakani kwa sasa Mohammadu Buhari alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupiga kura[…]

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Bashiru Ali amewatoa hofu Wazee wa Mkoa wa DSM kuwa Mchakato wa rasimu wa vyama vya siasa ambao ulijadiliwa na wabunge na kulalamikiwa na vyama vya upinzani hauna nia ya kuua Demokrasia.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Bashiru Ali amewatoa hofu Wazee wa Mkoa wa DSM kuwa Mchakato wa rasimu wa vyama vya siasa ambao ulijadiliwa na wabunge na kulalamikiwa na vyama vya upinzani hauna nia ya kuua Demokrasia nchini bali una lengo la kuimarisha vyama vya siasa na kuwajibika kwa wananchi na Taifa. Dkt.[…]

Watu 9 ambao ni wafanyakazi wa wizara ya ardhi, nyumba na makazi wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea kwenye kijiji cha Kikwawila wilaya ya Kilombero mkoni Morogoro.

Ajali hiyo imetokoea jana majiara ya saa 11 jioni baada ya dereva wa gari hilo lenye namba STK 9444 Land Cruiser kushindwa kulimudu akiwa katika mwendo mkali kutumbukia mtoni katika daraja la mto Kikwawila na kusabaisha vifo hivyo vya watu 9. Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo amesema kwenye[…]

Wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Kinyasi wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma wamefanikiwa kuwauwa majambazi wanne waliovamia katika kijiji chao na kupora zaidi ya Milioni 10.

Tukio hilo limetokea usiku wa tarehe 22 mwezi huu baada ya majambazi hao kuvamia kituo cha mafuta kijijini hapo kabla ya wananchi kuwashambulia kwa silaha za jadi, ambapo inaelezwa kuwa miili ya majambazi hao imehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya. Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi[…]

Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda amemtaka mmiliki wa Kiwanda cha Nyama cha Eliya Food Overseas Limited kukamilisha ujenzi wa Kiwanda hicho mpaka kufikia Mwezi Juni mwaka huu, ili kiwanda hicho kiweze kuzinduliwa rasmi Julai na kianze uzalishaji.

Waziri Kakunda amesema hayo mwishoni mwa wiki alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo eneo la Olendeki Kata ya Kimokouwa Wilayani Longido karibu na Mpaka wa Tanzania na Kenya, na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda hicho. Amesema hakuna sababu ya kuchelewesha ujenzi wa kiwanda ikizingatiwa kuwa wananchi wa eneo hilo wametoa kiwanja bure kwa mwekezaji huyo na[…]

Waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa ameagiza wataalam wa mamlala ya maji Tanga kufanya makadirio ya haraka kwa ajili ya kuboresha maji wa bwawa ili kuondoa kero ya maji kwa watumishi na wananchi wa kituo cha mpakani Horohoro.

Agizo hilo amelitoa baada ya kupokea taarifa ya utendaji wa wilaya mkinga ambayo imebainisha tatizo kubwa la ukosefu wa maji katika kituo cha mpaka wa horohoro mkoani Tanga. Amesema kutokana na ukubwa wa tatizo hilo Wizara ya maji ipo tayari kutoa fedha kwa miradi ya dharura kama huo wakati likitafutwa suluhisho la kudumu la kuwaptia[…]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia wananchi kwamba ahadi zote zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli katika maeneo mbalimbali nchini zitakuwa zimetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 90 ifikapo mwaka 2020.]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia wananchi kwamba ahadi zote zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli katika maeneo mbalimbali nchini zitakuwa zimetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 90 ifikapo mwaka 2020, kwani Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwahudumia wananchi na kuhakikisha huduma mbalimbali za kijamii kama maji, afya, nishati, elimu na miundombinu zinapatikana kwa uhakika. Waziri[…]

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kimeadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwake kwa kushiriki shughuli ya ujenzi wa jengo la ofisi ya chama hicho.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kimeadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwake kwa kushiriki shughuli ya ujenzi wa jengo la ofisi ya chama hicho katika ngazi ya wilaya huku kikitoa rai kwa vyama vingine vya siasa nchini kuwekeza katika falsafa ya sera bora badala ya kukumbatia dhana ya uanaharakati usio na tija[…]