Ubelgiji imesema itaendelea kudumisha Ushirikiano na Tanzania katika nyanja za kiuchumi na kimaendeleo ikiwa ni azma yake kuunga mkono mikakati inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano.

Ubelgiji imesema itaendelea kudumisha Ushirikiano na Tanzania katika nyanja za kiuchumi na kimaendeleo ikiwa ni azma yake kuunga mkono mikakati inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano ya kuimarisha na kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi pamoja na miradi mikubwa ya Kimaendeleo ikiwemo ya Miundombinu. Balozi wa ubelgiji hapa nchini Peter Van Acker pamoja na[…]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza viongozi na wazazi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro washirikiane kuhakikisha watu wote waliowapa mimba wanafunzi wanasakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza viongozi na wazazi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro washirikiane kuhakikisha watu wote waliowapa mimba wanafunzi wanasakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola, ambapo amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana, wanafunzi wa kike 57 walikatishwa masomo baada ya kupata mimba na hadi sasa kesi zilizofunguliwa ni sita[…]

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein amewataka wananchi kisiwani Pemba kuendelea kuiunga Mkono serikali katika kulinda miundombinu dhidi ya hujuma za baadhi ya wachache ili iweze kudumu.

Akizungumza na wananchi wa wilaya chakechake baada ya kuzindua kituo cha Afya Ngomeni, Dkt Shein ameahidi kufuatilia ili kujua gharama zilizotumika katika ujenzi wa kituo hicho. Mapema waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa , Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ Haji Omar Kheir alisema sehemu kubwa ya uchumi zanzibar[…]

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kupanda miti na kuitunza ili azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia Sekta ya Viwanda iweze kufikiwa.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo katika kongamano maalumu la mazingira mkoa ni Tabora ambalo limewakutanisha wadau mbalimbali ili kujadili namna ya kunusuru mkoa wa Tabora kutoka katika hatari ya kuwa jangwa. Katika hatua nyingine ameagiza kutumia rasilimali zilizopo kuwa na mfuko wa mazingira. Awali waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira[…]

Serikali mkoani Mwanza imewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kukamilisha ujenzi wa vituo hivyo kwa wakati ikiwa ni jitihada za kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Wakati ujenzi wa vituo hivyo ukiendelea kuhamasishwa kwa kuwashirikisha mafundi wa ndani kwenye ujenzi huo, mamia ya wakazi wa jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza, hivi karibuni wanatarajia kundokana na tatizo la ukosefu wa huduma ya afya. Tatizo hilo linatarajia kutoweka, baada ya ujenzi wa Hospitali ya Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema, kuelekea katika[…]

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI ya jijini Dar es Salaam wakishirikiana na madaktari kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Peking cha nchini China wameendesha zoezi la upasuaji wa ubongo pamoja na kuziba mshipa wa damu.

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI ya jijini Dar es Salaam wakishirikiana na madaktari kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Peking cha nchini China wameendesha zoezi la upasuaji wa ubongo pamoja na kuziba mshipa wa damu kwa wagonjwa wawili katika taasisi hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari wjijini Dar es Salaam , daktari bingwa[…]

Mkutano wa sita Baraza la Mawaziri kutoka nchi nane zinazounda bonde la mto Zambezi (ZAMCOM) unatarajiwa kufanyika February 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na waziri wa maji Prof. Makame Mbarawa wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jijini Tanga. Amesema mkutano huo wa baraza la mawaziri utapitia utekelezaji wa maagizo ya mkutano wa tano uliofanyika mwaka 2018 nchini Namibia, kupitia utekelezaji wa kamisheni kwa mwaka 2019 pamoja na kupitisha bajeti na mpangokazi wa mwaka 2019/20. Waziri[…]

Kesi ya mauaji ya watoto watatu inayowakabili watuhumiwa watatu mkoani Njombe leo imetajwa tena na kisha kuahirishwa hadi Machi 11, mwaka huu.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Njombe, MAGDALENA NTANDU amesema ameahirisha kesi hiyo kwa sababu bado upelelezi wa kesi unaendelea na watuhumiwa wote watatu wamerudishwa rumande… Watuhumiwa Joel Nziku, Nasson Kaduma na Alphonce Edward wanashitakiwa kwa mashitaka matatu ya mauaji ya watoto Godliver, Gilian na Gasper Nziku ambao walikuwa ni wakazi wa Kijiji cha[…]

Zoezi la kukusanya picha kwa ajili ya maadhimisho ya “miaka 55 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania”.

Mwaka huu China na Tanzania zinaadhimisha miaka 55 tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi. Ili kuadhimisha na kudumisha urafiki wa jadi kati ya nchi hizi mbili, Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China imeandaa shindano la kukusanya picha kwa ajili ya maadhimisho hayo. A。Tunachohitaji Picha zinazoonesha urafiki kati ya Tanzania na China, zinazoonesha[…]

Mashirika ya haki za binadamu nchini Nigeria yameripoti kuwa zaidi ya watu 40 wameuawa katika vurugu zilizoikumba Nigeria hapo jana wakati wa shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea kufuatia uchaguzi uliofanyika siku ya Jumamosi nchini humo.

Ingawa Taarifa hiyo iliyotolewa na Mashirika hayo ya haki za binadamu haijathibitishwa na vyombo vya Dola vya Nigeria lakini Polisi nchini humo imethibitisha kuwakamata watu zaidi ya 28 kutokana na kuhusika katika matukio ya vurugu yanayohusishwa na uchaguzi ambayo yamesababisha watu kadhaa kujeruhiwa huku wengine wakipoteza maisha. Rais wa sasa Muhammadu Buhari mwenye umri wa[…]