Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara, na taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu kuhakikisha zinapeleka vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinavyozingatia teknolojia mpya.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara, na taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu kuhakikisha zinapeleka vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinavyozingatia teknolojia mpya kulingana na mitaala ya serikali pamoja na kusambaza walimu katika vituo vya wenye uhitaji maalumu nchini ili kusaidia jamii hiyo kupata elimu bora inayokwenda na sambamba na soko la ajira.[…]

Mgombea urais wa chama tawala nchini Nigeria aliyekuwa akitetea kiti hicho Rais Muhammadu Buhari ameibuka mshindi wa uchaguzi uliofanyika Jumamosi Februari 23.

Kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi (INEC), Buhari amepata asilimia 56 ya kura zote zilizopigwa hivyo kumpa uhalali wa kuiongoza nchi hiyo ya Afrika magharibi kwa miaka mingine minne. Hata hivyo awali upinzani ulilalamikia kuwepo kwa njama za kuiba kura na kudai kwamba hautokubali matokeo hayo Habari zinasema Buhari ameshinda kwa[…]

Mkuu wa wilaya ya Wete Abeid Juma Ali amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Jeshi la kujenga uchumi -JKU– katika kuwatayarisha vijana kujenga uzalendo pamoja na maadili mema.

Akizungumza baada ya kushiriki zoezi la usafi wa mazingira katika hospitali ya wete, ikiwa ni shamrashamra ya miaka 42 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali amesema jeshi hilo limesaidia kuokoa nguvukazi na kuokoa uchumi wa nchi. Aidha amesema mafunzo yanayotolewa na Jeshi hilo limesaidia vijana kujiajiri wenyewe na[…]

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa suala la kupambana na rushwa lina umuhimu mkubwa katika maendeleo ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikizingatiwa kwamba vitendo hivyo vinazorotesha uchumi na maendeleo.

Dkt. Shein ameyasema hayo mjini Zanzibar wakati akizindua Mkutano wa Nne wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambapo kwa mwaka huu unafanyika mjini Zanzibar ambapo amesema kuwa kuwepo kwa Muswada wa rushwa katika mkutano wa Bunge hilo mwaka huu kuna umuhimu mkubwa kwani utasaidia katika kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikiathiri sana uchumi[…]

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ni miongoni mwa baadhi ya viongozi wa serikali, wanasiasa na wananchi wa kawaida waliojumuika katika maombolezo nyumbani kwa wazazi wa aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa CLOUDS MEDIA GROUP RUGE MUTAHABA.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ni miongoni mwa baadhi ya viongozi wa serikali, wanasiasa na wananchi wa kawaida waliojumuika katika maombolezo nyumbani kwa wazazi wa aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa CLOUDS MEDIA GROUP RUGE MUTAHABA aliyefariki dunia jana nchini AFRIKA KUSINI alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu RUGE MUTAHABA amefariki dunia baada ya kusumbuliwa kwa muda[…]

Halmashauri zote nchini zimetakiwa kujifunza kutekeleza miradi ya Kimkakati inayopatiwa ruzuku na Serikali, katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Halmashauri zote nchini zimetakiwa kujifunza kutekeleza miradi ya Kimkakati inayopatiwa ruzuku na Serikali, katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kuwa thamani halisi ya mradi wa Soko la kisasa utakaogharimu Sh. bilioni 17 hadi kukamilika kwake inaonekana. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea[…]