Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mbadala na Watu wazima , Mashavu Ahmada Fakih amesema uwepo wa vituo vya Mafunzo ya Amali vinawasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Bi Mashavu ameyasema hayo wakati akizungumza na walimu wapya wa kituo cha Mafunzo ya Amali Wingwi Wilaya ya Micheweni. Amesema vituo hivyo ni mkombozi wa vijana kwani huwapatia elimu ambayo itawasaidiaa kuweza kujiajiri wenyewe na kuacha kutegemea ajira kutoka serikalini. Aidha Bi Mashavu amewasisitiza kuisoma kanuni ya utumishi wa umma ili watambue wajibu na majukumu[…]

Katika kuhakikisha uvuvi haramu unaendelea kutokomezwa ndani ya Ziwa Victoria, Wizara ya mifugo na uvuvi imewapandisha kizimbani wavuvi haramu kumi na wanne, huku wavuvi saba wakihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Hii ni wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza inayoundwa na visiwa mbalimbali, ambayo wakazi wake hutegemea zaidi rasilimali ya uvuvi itokanayo na mazao ya samaki kama chanzo cha kujiingizia mapato, ili kujikimu na maisha ya kila siku. Wavuvi hao wamejikuta wakikabiliwa na hatia hiyo kupitia mahakama inayotembea ya kutokomeza uvuvi haramu, ili kulinda rasilimali zitokanazo na[…]

Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa imekamilisha mradi wa ufugaji nyuki wenye thamani ya shilingi milioni 60 iliyouanzisha.

Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa imekusudia kuondokana na kadhia ya utegemezi kwenye uendeshaji wa baadhi ya shughuli zake kama sehemu ya kutekeleza kwa vitendo falsafa ya ujamaa na kujitegemea mara baada ya kukamilika kwa mradi wa ufugaji nyuki wenye thamani ya shilingi milioni 60 iliyouanzisha. Akiongea wakati wa maadhimisho ya[…]

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ya Wilaya ya Njombe imesogeza mbele kesi namba tatu ya mwaka 2019 inayowakabili washitakiwa watatu wanaokabiliwa na kosa la mauaji ya Mtoto Rachael Malekela Mkoani Njombe kwa imani ya kishirikina.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ya Wilaya ya Njombe imesogeza mbele kesi namba tatu ya mwaka 2019 inayowakabili washitakiwa watatu Mariana Malekela, Edwin Malekela na Kalistus Ndiungwa wanaokabiliwa na kosa la mauaji ya Mtoto Rachael Malekela mwenye umri wa miaka saba ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Matembwe, Tarafa ya Lupembe mkoani Njombe kwa[…]

Wanafunzi ishirini na wa nne wa shule ya sekondari Mikindani iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wamejeruhiwa na radi huku mmoja akipoteza maisha.

Wanafunzi ishirini na wa nne wa shule ya sekondari Mikindani iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wamejeruhiwa na radi huku mmoja akipoteza maisha katika tukio hilo liliowakuta wakiwa darasani wakiendelea na masomo yao majira ya saa tatu asubuhi. Tukio hilo limetokea majira ya saa tatu asubuhi ambalo limewakumba wanafunzi wa kidato cha tatu A[…]

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imekutana na viongozi wa vyama vya siasa jijini Dar es salaam lengo likiwa ni kuwafahamisha wadau kuwa tume imekamilisha jukumu lake la kuhuisha na kuboresha kanuni za uchaguzi ambazo ziliandaliwa chini ya sheria mbili za mwaka 2008.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage amesema Taifa lipo katika maadalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, hivyo inafanya maboresho mbalimbali ikiwemo daftari la kudumu la wapiga pamoja na kuhakiki vituo vya kujiandikisha wapiga kura. Akizungumzia zoezi la uhakiki wa vituo amesema lililenga kuona[…]

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido amerejea leo nchini humo, baada ya ziara katika mataifa ya Amerika, na kushinikiza maandamano zaidi dhidi ya rais Nicolas Maduro.

Guaido ambaye alijiapisha kuwa rais wa watu na kuungwa mkono na mataifa ya Magharibi, yakiongozwa na Marekani, amepokelewa na maelfu ya wafuasi wake jijini Caracas. Kiongozi huyo amerejea nyumbani licha ya wasiwasi kuwa angekamatwa, baada ya kukiuka masharti ya Mahakama ya Juu, iliyokuwa imemzuia kutoka nje ya nchi hiyo. Hata hivyo Marekani imeionya serikali ya[…]