Rais wa Rwanda Paul Kagame amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo amekutana na Mwenyeji wake rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Rais Kagame amelakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki Prof.Palamagamba Kabudi akiambatana na viongozi wengine wa serikali wakiwemo baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa dar es salaam. Mara baada ya kuwalisili alipata fursa ya kuangalia vikundi vya ngoma vilivyoandaliwa[…]

Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa vituo vya Luninga na kituo cha Radio cha Clouds Fm cha Jijini Dar es Salaam Ephrahim Kibonde, aliyefariki Dunia majira ya alfajiri ya leo, unasafirishwa kuelekea Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Taarifa kutoka kwa rafiki yake aitwaye Baraka Chiru, zinaeleza kuwa kabla ya Marehemu Kibonde kufikwa na mauti, aliwasili Jijini Mwanza akitokea mjini Bukoba mkoani Kagera, baada ya kukamilisha mazishi ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba. Akiwa Jijini Mwanza taarifa hizo zinaeleza kuwa, Marehemu Kibonde alikuwa akijisikia vibaya kiafya, ambapo[…]

Serikali imesema itaendelea na jitihada zake kupambana na watu wote ambao wamekuwa wakiwarubuni na kushirikiana kwa nanma moja ama nyingine kuwaficha wahalifu wanowapatia mimba wanafunzi ambao wakati mwingine wamekuwa wakishirikiana na wazazi wa watoto hao.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametoa onyo hilo wakati wa hafla ya kukabidhi kadi 200 za matibabu za NHIF toto afya kadi kwa niaba ya waziri wa afya zilizotolewa na benk ya Stanbic kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima wakiwemo mia moja kutoka mkoa wa Arusha na mia moja[…]

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesitisha mpango wa mamlaka ya hifadhi ya jamii Burunge ( JUHIBU) wa kutaka kupiga mnada ng’ombe zaidi ya 700 waliokamatwa eneo la hifadhi.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesitisha mpango wa mamlaka ya hifadhi ya jamii Burunge ( JUHIBU) wa kutaka kupiga mnada ng’ombe zaidi ya 700 wa wafugaji waliokamatwa kwenye eneo la hifadhi hiyo iliyopo wilaya ya Babati Mkoani Manyara. Akizungumza na wananchi kwenye kijiji cha Maweni wilayani Babati mkuu wa Mkoa ameagiza pia kuachiwa[…]

Waziri Jaffo ameuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Uyui kusimamia mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo na kuhakikisha mhandisi anayetekeleza mradi huo anaongeza kasi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo ameuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Uyui kusimamia mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo na kuhakikisha mhandisi anayetekeleza mradi huo anaongeza kasi ili ifikapo mwishoni mwa mwezi juni ujenzi uwe umekamilika katika ubora unaotakiwa. Ni baada[…]

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ametoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa za viwanja vinavyoendelea kupimwa Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ametoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa za viwanja vinavyoendelea kupimwa Jijini Dodoma vikiwemo vya makazi, biashara na uwekezaji na kutoa angalizo kwa mamlaka husika kutoruhusu ujenzi holela ili jiji liwe la mfano. Dkt. Mahenge ametoa wito huo baada ya kutembelea miradi ya upimaji wa viwanja katika kata[…]

Wanajeshi wa India na Pakistan wameshambulia vituo vya kijeshi na vijiji kwenye mpaka wao wenye shughuli nyingi za kijeshi wa jimbo linalogombaniwa la Kashmir, katika machafuko mapya licha ya nchi hizo mbili kuongeza juhudi za kutuliza mvutano.

Wanajeshi wa nchi hizo wametuhumiana kwa kuanzisha mashambulizi katika eneo hilo ambapo mpaka sasa hakuna habari zozote zilizotolewa mara kuhusiana hasara iliyotokea. Hofu imekuwa kubwa tangu ndege ya India iliporuka katika anga ya Pakistan wiki iliyopita ikifanya kile ambacho India ilisema ni shambulizi dhidi ya wanamgambo waliohusika na mlipuko wa bomu wa kujitoa mhanga Februari[…]

Kiwanja cha Ndege Arusha ambacho ni cha Tatu hapa Nchini kwa uingizaji wa mapato, kinakabiliwa na uchakavu katika maeneo mbalimbali, ekiwemo sehemu ya kiungo cha kurukia ndege, jambo linalosababisha baadhi ya ndege kubwa kushindwa kutua na kuruka.

Kiwanja cha Ndege Arusha ambacho ni cha Tatu hapa Nchini kwa uingizaji wa mapato, kinakabiliwa na uchakavu katika maeneo mbalimbali, ekiwemo sehemu ya kiungo cha kurukia ndege, jambo linalosababisha baadhi ya ndege kubwa kushindwa kutua na kuruka eneo linalohitaji ukarabati kwa haraka. Katika Taarifa yake mbele ya mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na[…]