Serikali ya Mkoa wa Dsm imesema itaendelea kuenzi na kuthamini Mchango na wanawake katika Maendeleo lakini pia kusimamia na kuwachukulia hatua wanaume au watu wanaonyanyasa au kuwadhalilisha wanawake.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda akizungumza wakati wa maadhimisho ya wanawake jijini dsm ambapo maelfu ya wanawake kutoka wilaya zote za jiji la dsm walijitokeza amesema katika mkoa wa dsm atahakikisha vitendo vya udhalilishaji au uonevu kwa wanawake vinakomeshwa. Aidha Makonda pia amewageukia wanaume wanaowarubuni wasichana wadogo wakiwemo wanafunzi na kuwapa mimba wajiandae[…]

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mazingira mazuri kwa kuimarisha miundo mbinu mbali mbali na kuendeleza huduma za jamii mijini na vijijini.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mazingira mazuri kwa kuimarisha miundo mbinu mbali mbali na kuendeleza huduma za jamii mijini na vijijini ikiwa ni pamoja na kuimarisha mapambano dhidi ya matendo ya udhalilishaji. Akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake , Bi Mwanamwema Shein[…]

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani wafanyakazi wa kampuni ya Africa Media Group inayomiliki kituo cha Channel Ten na Magic Fm Radio wameonyesha uwezo wao kwa kufanya kazi katika vitengo vyote vya kampuni hiyo.

Mapema asubuhi timu ya wafanyakazi hao ilijipanga ikiwemo kuendesha kipindi cha baragumu live kinachorushwa kupitia Channel Ten na kipindi cha morning Magic kinachorushwa kupitia Magic Fm na kusoma taarifa zote za habari. Baadhi ya wafanyakazi wanawake akiwemo Mwanahamisi Bashiri Mwenda wa Magic FM na KISSA MWAIPYANA wa Channel Ten wamesema kuwa uongozi uliamua kuwaachia wafanyakazi[…]

Mgogoro ulioibuka katika eneo la mgodi wa madini ya Roadlight katika kijiji cha Naepo eneo la Mirerani wamemuomba rais Magufuli kuingilia kati.

Kutokana na sintofahamu iliyoibuka katika eneo la mgodi wa madini ya Roadlight katika kijiji cha Naepo eneo la Mirerani, ambapo kampuni mbili za wachimbaji wadogo wote wakimiliki leseni halali za kuchimba katika eneo hilo mmoja wa wamiliki wa mgodi huo tangu mwaka 2002 bwana Methew Massawe anayedai kuvamiwa eneo lake,amemuomba rais Magufuli kuingilia kati mgogoro[…]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kifo cha aliyekuwa Mtangazaji Muandamizi wa kituo cha redio cha Clouds, Ephraim Kibonde ni pengo kubwa kwa Taifa, Clouds Media Group na tasnia ya habari kwa ujumla.

Ameyasema hayo alipokwenda kuhani msiba wa Mtangazaji Muandamizi kituo cha redio Clouds, Kibonde kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mbezi Beach Dar es salaam. Waziri Mkuu amesema marehemuKibonde enzi za uhai wake ameshirikiana vizuri na Serikali katika shughuli mbalimbali, hivyo amewaomba wananchi waendelee kushikamana na kuifariji familia. Kadhalika, Waziri[…]

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 2 hapa nchini Tanzania na kurejea nchini kwake, baada ya hapo jana kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 2 hapa nchini Tanzania na kurejea nchini kwake, baada ya hapo jana kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini[…]