Watuhumiwa watatu kati ya watano wameuawa baada ya jeshi la polisi kuwabaini wakitekeleza tukio la unyanganyi kwa kutumia silaha za jadi ikiwemo Mapanga na Marungu kuteka gari aina ya Land Cruiser ambalo linahudumia wakimbizi katika kijiji cha Nyarulanga kata ya Busunzu wilayani Kibondo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma Martin Otieno amesema Machi 10/2019 majira ya saa mbili asubuhi majambazi hao waliteka gari aina ya land cruiser linalomilikiwa na shirika la Good neighbour na kupora mali mbalimbali ikwemo laptop,simu na fedha tasliumu ambapo thamani ya vitu vinadaiwa kuwa ni shilingi 3,334,000. Aidha kamanda Otieno[…]

Chama cha Mawakala wa forodha nchini Tanzania -TAFFA kimepata pigo baada ya Rais wa Chama hicho Steven Ngatunga kufariki dunia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua ghafla siku chache alipotoka jijini Dodoma kushiriki kikao cha kikazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Chama cha Mawakala wa Forodha TAFFA Otieno Igogo amesema Marehemu Ngatunga ameaga dunia ikiwa ni miezi miwili baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya Urais wa Mawakala katika nchi za Afrika mashariki na mashariki ya kati. Aidha Bw,Igogo amesema kuwa Alhamisi[…]

Wadau mbalimbali wametakiwa kuunganisha nguvu ili kuhakikisha kiwango cha maambukizi ya malaria Mkoani Tabora kinashuka kutoka asilimia 11 na kufikia walau kile cha Kitaifa cha asilimia 7 ikiwa ni jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo.

Ni ufunguzi wa jukwaa la mawasiliano ya Afya NAWEZA ambalo linahusika zaidi na watu wazima kwa mikoa ya Tabora, Arusha na Singida. Akizindua jukwaa hilo mkuu wa mkoa wa Tabora AGGREY Mwanri anasema kuna haja ya kuunganisha nguvu kati ya serikali na wadau mbalimbali katika kutoa elimu ili kukabiliana na magonjwa yanayoikabili jamii ikiwemo malaria[…]

Shirika kuu la utangazaji la China CMG lajitahidi kufanya uvumbuzi na kujijenga kuwa chombo kikubwa cha habari cha aina mpya.

Shirika kuu la utangazaji la China CMG linajitahidi kutumia teknolojia mpya na kufanya uvumbuzi wa kuunganisha mbinu za kisasa za utangazaji kupitia majukwaa mbalimbali, ili kutangaza kwa ufanisi maamuzi ya Chama na maoni ya wajumbe kwenye Mikutano miwili inayoendelea kufanyika hapa Beijing. Wakati wa kuripoti Mikutano mwili ya mwaka huu, Shirika kuu la utangazaji la[…]

Teknolojia za kisasa kuleta mwelekeo mpya wa kuchanganywa kwa vyombo vya habari.

Vyombo vikuu vya habari vya China ikiwemo Shirika Kuu la Utangazaji la China vimetumia teknolojia ya kisasa katika kukusanya na kutangaza habari za mikutano ya Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya kisiasa la China inayofanyika hapa Beijing. Wajumbe wanaohudhuria mikutano hiyo wamesema, teknolojia hizo zitaleta mwekeleo mpya wa kuchanganywa na kuendelezwa kwa vyombo[…]

Jeshi la Polisi katika wilaya ya kipolisi ya Kawe mkoa wa Dar es Salaam limekamata shehena ya Sukari pamoja na Mafuta ya kula iliyokuwa ikiingizwa Tanzania Bara kimagendo kupitia bandari Bubu -Mbweni kutoka visiwani Zanzibar.

Aidha jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wanne wanaodaiwa kuwa vinara wa kuingiza bidhaa za magendo kupitia ukanda huo wa Pwani ya Mbweni na kusafirisha bidhaa hizo kwa kutumia ng’ómbe nyakati za Usiku. Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amesema Ukanda huo wa Pwani ya Mbweni umekuwa na changamoto kubwa ya[…]

Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabili changamoto ya usawa wa kijinsia, ambapo imehakikisha kwa vitendo kwamba wanawake wanapata fursa na usawa unaostahili katika vyombo vikubwa vya maamuzi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Radio Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kwa mara ya kwanza Tanzania imepata Makamu wa Rais Mwanamke, ikiwa ni jitihada ya kuondoa changamoto hii ya usawa wa kijinsia, ambayo bado ni kubwa duniani. Waziri Ummy Mwalimu[…]