Mamlaka ya kuratibu safari za anga za Marekani, FAA, imesema haitasimamisha safari za Ndege aina ya Boeing 737 Max, kufuatia ajali ya Ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia iliyosababisha vifo vya watu 157.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kaimu afisa mkuu wa mamlaka hiyo, Dan Elwell, alisema Jumanne kwamba uchunguzi uliofanywa kufikia sasa, haujabaini hitilafu yeyote katika mfumo wa Ndege hizo na kwa hivyo haoni haja ya kusitisha safari zake. Ajali hiyo imesababisha baadhi ya mashirika ya ndege ya nchi kadhaa kusitisha safari za ndege[…]

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Urusi ulioongozwa na Mjumbe Maalum wa Rais wa Urusi katika masuala ya Afrika ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mikhail Bogdanov, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa ushirikiano na uhusiano mzuri kati ya Tanzania na nchi hiyo na amemhakikishia kuwa Serikali anayoiongoza inatambua umuhimu wa uhusiano huo na kwamba itauendeleza na kuukuza zaidi hususani katika masuala ya biashara, uwekezaji, utalii na utoaji wa huduma za kijamii kama vile afya, elimu na miundombinu. Kwa[…]

Timu iliyoundwa kuchunguza chanzo cha ajali iliyotokea maeneo ya Senjele wilayani Mbozi mkoani Songwe na kusababisha vifo vya watu 19 February 21 mwaka huu imewasilisha ripoti yake ambayo imebaini kuwa chanzo kikubwa cha ajali hiyo ni ubovu wa lori ambalo lilikuwa likitokea nchini Zambia.

Ajali hiyo ilihusisha malori mawili na bus la abiria aina ya Coaster mali ya kampuni ya Komkya. Akiwasilisha ripoti ya uchunguzi wa ajali hiyo iliyoundwa chini ya Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Fortunatus Musilimu, Katibu wa kamati hiyo KISBERT KAPONDO ametaja chanzo cha ajali hiyo ambayo iligharimu maisha ya watanzania 19. Mkuu wa[…]

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umesema hautamvumilia mtu au kikundi cha watu watakaotumia lugha ya matusi au udhalilishaji dhidi ya viongozi.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umesema hautamvumilia mtu au kikundi cha watu watakaotumia lugha ya matusi au udhalilishaji dhidi ya viongozi badala yake umetoa rai kwa wananchi kuunga mkono juhudi zinachukuliwa na serikali ya awamu ya 5 katika kuimarisha uchumi. Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana[…]

Watumishi wawili wa idara ya afya wa Zahanati ya Mutundu Wilaya ya Chato Mkoani Geita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kuuza na kutorosha dawa za serikali kwa mfanyabiashara mmoja Mkazi wa Buseresere.

Watuhumiwa hao ni Mganga Mfawidhi waa zahanati hiyo Thobias Kagomana, muuguzi Boniface Paschal ambaye pia ni mtunza stoo pamoja na Mfanyabiashara Balamius Kamugisha. Taarifa za Jeshi la polisi zinasema kuwa Mtuhumiwa Balamius Kamugisha amekamatwa katika Kata ya Buseresere kwa kosa la kukutwa na dawa za Binadamu nyumbani kwake kinyume na sheria, huku ikidaiwa kuwa amekuwa[…]

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Walioapishwa ni pamoja na Hamida Mussa Khamis ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja, Khalid Abdalla Omar anayekuwa Naibu Katibu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ pamoja na Omar Said Ameir anayekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar. Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Spika[…]

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ili kuibadili Afrika Viongozi wake lazima wawekeze kwa Vijana na Watoto.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia kwenye mkutano wa Africa Now Summit 2019 jijini Kampala nchini Uganda. Amesisitiza kwamba viongozi lazima wawekeze kwenye Lishe bora ya watoto wanaozaliwa na kuhakikisha mifumo ya elimu inalenga kutoa elimu bora na zenye kukuza vipaji ili kwenda sambamba na ulimwengu wa teknolojia. Aidha Makamu wa Rais amesisitiza Afrika[…]