Serikali kupitia Wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, inatarajia kutatua mgogoro wa wananchi wanaodaiwa kuvamia maeneo ya uwanja wa ndege wa Mwanza kwa kuwalipa fidia, ili kupisha upanuzi wa uwanja huo, unaotarajiwa kujengwa kwa hadhi ya kimataifa.

Uamuzi wa Serikali wa kutaka kuwalipa fidia wananchi hao, vilevile utasaidia kutatua kilio kuhusu hatma ya wananchi wa maeneo hayo, baada ya kudaiwa kuwa maeneo wanayoishi waliyavamia kinyume cha sheria. Akiwa katika ziara ya ukaguzi wa maeneo yanayozunguka uwanja wa ndege wa Mwanza, Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano mhandisi Isack Kamwelwe, amesema ziara yake[…]

Kufuatia taharuki iliyowapata wakazi wa jiji la Arusha kwa takribani wiki moja na nusu sasa baada ya baadhi yao kulalamikia kusumbuliwa na magonjwa ya tumbo, Mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo ameingilia kati na kuagiza wataalam wa afya kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha malalamiko hayo ili hatua stahiki zichukuliwe.

Gambo ambae amelazimika kutembelea makazi ya wananchi katika eneo la Pangani ya chini na daraja mbili jijini humo yanayodaiwa kukumbwa na mlipuko huo na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo,ambapo yeye binafsi na viongozi wengine wakaamua kujiridhisha usalama wa maji hayo kwa kuyanywa. Hata hivyo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya mkoa ya mountmeru Dkt.[…]

Watanzania wameaswa kujiwekea utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara na kuepuka matumizi ya dawa za kutuliza maumivu kiholela zinazotajwa kuwa miongoni mwa visababishi vya ugonjwa wa figo.

Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto, Dkt. Faustine Ndungulile wakati akizungumza na wanahabari kuhusu siku ya figo duniani inayoadhimishwa kila Machi 14. Akizungumza katika mkutano huo, Naibu waziri Dkt. Ndungulile amesema kuwa miongoni mwa visababishi vya ugonjwa wa figo nchini ni pamoja na kutofanya[…]

Mchumi na mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Honest Prosper Ngowi amepongeza makadirio ya Bajeti kwa mwaka 2019/20 pamoja na vipaumbele vyake pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kukuza mapato ya ndani.

Mchumi na mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Honest Prosper Ngowi amepongeza makadirio ya Bajeti kwa mwaka 2019/20 pamoja na vipaumbele vyake pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kukuza mapato ya ndani ili nchi iweze kujitegemea na kupunguza au kuachana kabisa na fedha za wahisani. Akitoa uchambuzi wa makadirio ya bajeti hiyo Profesa Honest Prosper[…]

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tshisekedi amewasamehe takriban wafungwa 700 wa kisiasa waliofungwa jela na utawala wa mtangulizi wake, Joseph Kabila.

Tshisekedi alisaini amri ya rais ya kuwasamehe wafungwa hao jana na kutimiza ahadi aliyoitoa mwanzoni mwa mwezi huu, kwamba hilo ni moja kati ya mambo atakayoyafanya katika siku zake 100 za kwanza madarakani. Miongoni mwa walioachiwa huru ni Firmin Yangambi, aliyehukumiwa mwaka 2009 kifungo cha miaka 20 gerezani kwa makosa ya kutishia usalama wa taifa.[…]

Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kusitisha mara moja safari za ndege za Boeing chapa 737 MAX 8, baada ya ndege kama hiyo ya Ethiopia kuanguka Jumapili iliyopita na kuwaua watu wote 157 waliokuwemo ndani.

Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kusitisha mara moja safari za ndege za Boeing chapa 737 MAX 8, baada ya ndege kama hiyo ya Ethiopia kuanguka Jumapili iliyopita na kuwaua watu wote 157 waliokuwemo ndani. Akizungumza na waandishi habari katika Ikulu ya Marekani, Trump amesema amezipiga marufuku ndege hizo kuruka kutokana na kuongezeka kwa shinikizo[…]