Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kambi ya wachezaji wa timu ya Taifa na kuwaeleza kwamba Serikali na wananchi wana matumaini makubwa kwa timu yao, hivyo wahakikishe wanapata ushindi katika mechi yao dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda leo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amewaeleza wachezaji hao kuwa Serikali ina imani nao na kwamba wasiwe na wasiwasi kwa sababu hawana tofauti yoyote na wachezaji wa timu nyingine duniani, hivyo akawataka wakapigane kufa na kupona ili kupata ushindi na hatimaye kufuzu. Taifa Stars kupitia Nahodha wake Mbwana Samata wamemwahidi Waziri Mkuu kwamba watapigana kufa na kupona kuhakikisha kwamba[…]