Waziri mkuu Kassim Majaliwa amezindua maabara ya kisasa ya uchunguzi wa mionzi yenye viwango vya kimataifa.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa serikali wa kujenga maabara ya kisasa ya uchunguzi wa mionzi yenye viwango vya kimataifa ni kuhakikisha inaimarisha ulinzi na usalama wa nchi na mipaka yake yote dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa hapa nchini kupitia mionzi. Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi ya maabara hiyo katika[…]

Katibu Mkuu CCM Dkt. Bashiru Ally leo amekutana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wapigania Uhuru wa Frelimo (Veterans) nchini Msumbiji .

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally leo amekutana na Kufanya Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Wapigania Uhuru wa Frelimo (Veterans) nchini Msumbiji katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Channel Ten Dkt, Bashiru Ally amesema Ujumbe huo ambao upo nchini kwa ziara ya siku tatu[…]

Zikiwa zimesalia siku chache kuanza kwa zoezi la usajili wa kadi za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole.

Zikiwa zimesalia siku chache kuanza kwa zoezi la usajili wa kadi za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole Mei mosi mwaka huu, baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wameonyesha wasiwasi kuwa huenda watashindwa kupata huduma hiyo kutokana na kutokuwa na vitambulisho vya Taifa ambavyo vitatumika katika usajili huo. Wakizungumza na[…]

Mawakili wa Upande wa Jamhuri kesi ya Mkurugenzi wa UDART wameiomba Mahakama ahirisho fupi.

Mawakili wa Upande wa Jamhuri katika kesi inayowakabili ya aliyekuwa Mkurugenzi wa UDART Robert Kisena na wenzake wameiomba Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ahirisho fupi kwa ajili ya kufanyia kazi maelezo ya mwendesha mashtaka wa serikali DPP huku wakidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Akiwasilisha ombi hilo mbele ya hakimu[…]

APRM imebaini mafanikio makubwa eneo la kuimarisha demokrasia, usimamizi wa uchumi na huduma za kijamii.

Mpango wa tathmini ya utawala bora katika Bara la Afrika APRM umebaini kuwepo kwa mafanikio makubwa hapa nchini katika eneo la kuimarisha demokrasia, usimamizi wa uchumi na huduma za kijamii. Aidha mpango huo unatajwa kufanya vema katika maeneo mengine yakiwemo ya uendeshaji wa mashirika ya biashara ambapo Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika eneo la[…]

Rais Dkt. Magufuli amezindua Kiwanda cha Nafaka cha JKT-Mlale Songea mkoani Ruvuma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli amezindua Kiwanda cha Nafaka cha JKT-Mlale Songea mkoani Ruvuma ambacho kimegharimu shilingi milioni 414.77 ambacho kitachakata mahindi tani 5280 kwa mwaka. Akizindua kiwanda hicho Rais Dkt. Magufuli amesema azma ya serikali ya awamu ya tano ni kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa kati kupitia sekta[…]