Samaki Chongowe ameonekana katika eneo la Kinowe Pemba, wananchi wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya Samaki huyo.

Samaki Mkubwa mwenye Urefu wa zaidi ya Mita 15, Upana Mita Saba anayejulikana kwa jina maarufu “Chongowe” ameonekana katika eneo la Kinowe , Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo wananchi wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya Samaki huyo ili kunusuru kutokea Madhara. Akizungumza na wananchi katika bandari ya Kinowe Wilayani Micheweni, Kaimu Afisa Mkuu[…]

Raia wa Ukraine wataamua juu rais ajaye wa taifa hilo katika duru ya pili ya uchaguzi.

Raia wa Ukraine wataamua juu rais ajaye wa taifa hilo katika duru ya pili ya uchaguzi ingawa ripoti zinasema mchekeshaji Vladmir Selenski alipata kura nyingi zaidi katika duru ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika jana Jumapili. Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 41 alishindwa kupata wingi unaohitajika kwa kupata karibu asilimia 30. Hivyo Selenski atakabiliana na[…]

Wakaazi wa Beni, Butembo na Yumbi wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa wabunge DRC.

Wakaazi wa Beni, Butembo na Yumbi wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliyofanyika jana¬† Machi 31 baada ya kuahirishwa miezi mitatu iliyopita. Uchaguzi huo umefanyika katika maeneo hayo matatu, baada ya Tume ya Uchaguzi (CENI) kuchukuwa hatua ya kusogeza mbele uchaguzi katika maeneo hayo kutokana na sababu za kiusalama na afya. Wapiga kura katika[…]