TFF imeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Uhlsport kwa ajili utengenezaji wa jezi zitakazotumiwa na timu ya taifa – ”Taifa Stars”

Shirikisho la soka nchini TFF limeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Uhlsport kwa ajili utengenezaji wa jezi zitakazotumiwa na timu ya taifa ya Tanzania ”Taifa Stars” kuelekea mashindano ya mataifa ya Afrika AFCON mwaka huu nchini Misri. Akizungumzia mkataba huo Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Wallace Karia, amesema jezi hizo[…]

Wazalishaji Mifuko mbadala watakiwa kuomba Leseni.

Shirika la Viwango Tanzania TBS limewataka wazalishaji wote wa mifuko mbadala pamoja na waagizaji wa mifuko hiyo kutoka nje kuwasilisha upya maombi ya kupatiwa leseni, baada ya shirika hilo kusitisha uhuishaji wa leseni za awali zilizoruhusu uzalishaji wa mifuko ya plastiki. Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika hilo Bw. Lazaro Msalalaga amesema hatua hiyo[…]

Serikali kuwachukulia hatua wahujumu Uchumi.

Katika kuhakikisha Taifa linanufaika na rasilimali zake, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeonya kuwachukulia hatua kali za kisheria, watu watakaothibitika kujihusisha na vitendo vya uhujumu uchumi, ikiwemoBiashara haramu ya utoroshaji wa madini nchini. Serikali imetoa onyo hilo leo wakati ikikabidhiwa madini na mali nyingine, zilizotaifishwa kutokana na kesi ya uhujumu uchumi namba moja ya mwaka[…]

Uhuru Media yafuturisha Wafanyakazi wake.

Kampuni ya Uhuru Media Group imefuturisha wafanyakazi wake kutoka kwenye kampuni zake tanzu ikiwamo Africa Media Group Ltd, inayomiliki vituo vya channel ten, Magic FM, DTV na CTN. Akizungumza na wafanyakazi hao mara baada ya kufuturu, mwenyekiti mwenza wa Uhuru Media Group Dkt Abdullah Juma Saadallah… amewasisitizia wafanyakazi hao kuendeleza umoja na mshikamano kwani hiyo[…]

Mwisho wa Mifuko ya Plastiki.

Kufuatia katazo la matumizi ya mifuko ya plasiki nchini wafanyabiashara mbalimbali mkoani Dodoma wameiomba serikali iongeze nguvu ya uzalishaji wa mifuko mbadala ili kukidhi mahitaji yaliyopo. Rai hiyo imetolewa baada ya ziara iliyofanywa na ofisi ya makamu wa raisi kwa kushirikiana na ofisi ya mazingira ya jiji la Dodoma, iliyokuwa na lengo ilikuwa na lengo[…]

Wananchi wametakiwa kutumia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kama fursa.

Wananchi wametakiwa kutumia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kama fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vya kuzalisha mifuko mbadala hatua ambayo itasaidia kuwapatia kipato na hatimaye kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya mifukpo hiyo. Kutokana na madhara kadha wa kadha yanayotokana na matuimizi ya mifuko ya plastic ikiwa ni pamoja na kusababisha[…]

Serikali inakusudia kuanza ujenzi wa reli ya kisasa itakayoanzia katika bandari ya Mtwara hadi Mbamba bay mkoani Ruvuma.

Serikali inakusudia kuanza ujenzi wa reli ya kisasa itakayoanzia katika bandari ya Mtwara hadi Mbamba bay mkoani Ruvuma,reli ambayo inatarijiwa kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kwa ukanda wa kusini kupitia sekta ya usafirishaji ambapo pamoja na usafirishaji wa bidhaa zingine chuma na makaa ya mawe yanatarajiwa kusafirishwa kwa wingi kupitia reli hiyo. Hapa ni[…]