Kijana anasa kwenye Miamba ya Mawe akisaka Madini.

Vikosi vya ulinzi na usalama likiwemo jeshi la wananchi, polisi, uhamiaji, zimamoto na uokoaji kwa pamoja leo vimekuwa katika juhudi za kumnasua kijana mwenye umri wa miaka 24 aliyefahamika kwa jina la Elias Marwa mkazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara aliyenasa katikati ya mwamba wa jiwe kubwa wakati akisaka madini chini ya ardhi.

Kwa mujibu wa Familia ya Kijana Elias Marwa aliyenasa kwenye mwamba tangu tarehe nne mwezi wa tisa 2019 majira ya saa nnne asubuhi inasemekana kuwa kijana Elisas Marwa amekuwa akiingia mara kwa mara kwenye miamba hiyo kusaka madini ila siku hiyo alichelewa kurejea hali iliyompa mashaka mdogo wake Ramadhani Marwa aliyekuwa akifanya naye kazi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa mara Salumu Mohamedi amesema kuwa zoezi la uokoaji limechukua muda mrefu kwa kuwa mwili upo mbali chini ya ardhi hivyo wanalazimika kutuumia baruti kupasua mawe yaliyopo juu ili kufanikisha kumtoa kijana huyo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lajadili Muswada wa marekebisho wa Sheria.

Read Next

Waendesha Bodaboda Morogoro waondolewa eneo lisilo rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!